Wafanyakazi wa zimamoto New York City wakiwa nje ya kanisa la Mt.Patrick kabla ya kuanza kwa misa ya kuwakumbuka waliopatwa na maafa Sept 11,2001 kwenye ghorofa pacha za World Trade Center,Mjini Humo.
Wafanyakazi na watu mbali mbali waliojumuika pamoja kwenye misa hiyo iliyofanyika katka kanisa la Mt.Patrick lililopo barabara ya 5 NYC
Meya wa mji wa New York,Michael Bloomberg akisema machache huku kadinali Edward Egan akimsikiliza hii ni wakati wa misa ya kuwakumbuka waliopata na maafa Sept 11,2001 wakiwemo wafanyakazi wa zimamoto wa mjini humo.
wakina mama waliokumbatiana wakionekana kulengwa na machozi kwa kukumbuka maafa yaliyotokea Sept 11,2001
Mfanyakazi wa Zimamoto,New York City akilengwa na machozi alipokua akimsikiliaza moja ya mtoto wa mfanyakazi wa Zimamoto wa NYC aliyekua mmoja wa maelfu waliopoteza maisha Sept 11,2001 ambapo leo ni miaka 10,misa ya kuwakumbuka waliopatwa na maafa hayo ilifanyika katika kanisa la Mt. Patrick lililopo barabara ya 5 njini humo
Kristen Ross aliyetokea New South Wales(Autralia) Fire Brigade akiwa nje ya kanisa la Mt.Patrick,Kristen ni mmoja ya mamia ya Wazimamoto kutoka sehemu mbali mbali Dunian waliokuja New York City kuungana na wazimamoto wenzao katika kuwakumbuka waliopata maafa Sept 11,2001
Watu mbali mbali wakiwa nje ya kanisa la Mt.Patrick mjini NYC wakifuatilia misa ya kumbukumbu ya maafa ya Spt 11,2001,mjini humo.(picha kwa hisani ya Mario Tana/Getty Image North America)
No comments:
Post a Comment