Polisi wakijaribu Kuzuia Ghasia katika eneo hilo na kufukuza Wamachinga
Baadhi ya wananchi wakiwa wameokoka katika eneo hilo
Wamachinga Mbali mbali wakikimbia katika eneo la tukio wakati wa machafuko hayo yamepamba moto
Watu Mbali Mbali wakiwa wanakimbia ili kujiokoa na Hatari katika eneo hilo
Wamachinga wakiwa Tayali kwa ajili ya Kupambana na FFU wakati wa tukio hilo
Picha zote na Mpiga picha wetu maalum
Mbeya Yetu Blog
Mimi nashangaa sana serikali yetu kweli ishukuru angalau hawa watu wanajaribu kujitafutia maisha maana kazi hazipatikani kirahisi uwe na kisomo au usiwe na kisomo yote ni moja kwa nini serikali isitafute eneo kwa ajili ya hawa watu ambao watanajitafutia maisha hawataki kuwa waporaji kwa nini serikali isijenge eneo maalum na kuwachaji kodi kidogo kwa ili waweze kuimarisha hilo eneo.
ReplyDeleteNi kweli kabisa uliyetangulia umeongea la maana kabisaa. Walivyotamka kuwa Wamachinga hao hawakuwa na mpango wowote wa Kupora au Kumdhulu mwananchi yeyote zaidi ya kujitetea kwa ajili ya sehemu wanazojipatia Kula yao na Familia zao. Serikali angalieni Maswala ya Wananchi wenu kama hao, siyo mnajiangalia nyie Wakubwa wa Serikali na Safari za kwenda Nje ya Nchi kila siku kwa ajili ya Mahitaji yenu nyie wenyewe, mnajisahau kabisa kusaidia wananchi wadogowadogo wanaojitahidi kujisaidia kwani Serikali yetu haiwakumbuki kabisa watu wa Maisha ya hali ya chini. Naipenda nchi yangu ila Fanyeni mambo ya kuendeleza nchi yetu siyo kujiendeleza nyinyi wenyewe.Usome, Usisome, Kazi ni za shida tu. Pesa yote inaishia kwa Wabunge kujinufaisha wao wenyewe. Mungu Ibariki Tanzania. Tunakulilia.
ReplyDelete