TUPO kwenye kipindi kigumu. Mapenzi sahihi yanapigwa vita, mataifa makubwa yaliyoendelea yanahimiza mapenzi feki yasiyo na baraka kutoka kwa Mungu. Yanataka ziwepo ndoa za mashoga na wasagaji. Tumuombe Mola atuepushe na balaa hilo.
Kila mtu anapenda kuonewa wivu ili awe na uthibitisho kuhusu mvuto wake. Anahitaji kujua kama anapendwa na kwamba yupo anayemjali, ambaye asipokuwa karibu yake, atamsumbua kwa maswali kama,
“upo wapi? Unafanya nini? Na nani?”Kila mtu anapenda kuonewa wivu ili awe na uthibitisho kuhusu mvuto wake. Anahitaji kujua kama anapendwa na kwamba yupo anayemjali, ambaye asipokuwa karibu yake, atamsumbua kwa maswali kama,
Asije kukudanganya mtu kuwa hapendi kuonewa wivu. Nimelazimika kutoa neno hili kwa sababu kumekuwa na tabia ya watu kuongopeana kuwa hawapendi usumbufu. Wengine wanajaza hekima dhaifu za mapokeo ya kizamani: “Mimi mpenzi wangu Mzungu, hanibani wala nini!”
Je, ni kweli kuwa Wazungu hawaoni wivu? Unajua ni kwa nini Chris Brown alimpa kipigo Robyn Rihanna Fenty? Uhusiano wa kimapenzi una nguzo zake, na moja kubwa ni jinsi wewe unavyomjali mwenzi wako na kumfanya ajione mwenye thamani kuu.
Hujui kuwa mpenzi ni mali yenye thamani? Kama unatambua hilo ni vizuri kuilinda kwa gharama yoyote. Abiria anahimizwa achunge mzigo wake, iweje wewe usidhamirie kumhifadhi mwandani wako? Akili itulie kichwani kwako, wapo wanaolia kwa kuzidiwa kete na marafiki zao.
Hawajui kuwa walicheza ‘faulo’ ndiyo maana wakajikuta wanawekwa pembeni. Hutaki kumuonesha unamjali kwa kipimo kinachostahili, matokeo yake rafiki yako anachukua nafasi. Hujui kumuuliza kulikoni anapokuwa mnyonge, mwenzako anatimiza hilo.
Mapenzi ni sanaa ambayo inamtaka mtu aishi ndani ya mwenzi wake. Uwe mwepesi kujua yaliyomo kwenye fikra zake. Katika ‘malavidavi’ epuka usistaduu, ubrazameni au ugumu. Unahitaji kuwa rahisi kwa mwenzi wako na umfanye ajione hajakamilika bila uwepo wako.
Unaweza kufanya kitu ambacho wewe utakiona ni kidogo lakini kwa mwenzako kikawa kimemmaliza kabisa. Fikiria unaamka asubuhi na mapema, unamuamsha ili awahi kazini. Anakuta umemuandalia kila kitu, mnakwenda kuoga pamoja, mnapata kifungua kinywa mezani halafu mnatengana kwa muda kwa sababu mnawajibika ofisi tofauti.
Si kwa kuangalia jinsi. Fikiria pia wewe ni mwanaume ambaye unafanya kitu kumfurahisha mwenzi wako. Unaamka mapema na kunyoosha nguo za mkeo. Unamuamsha na anakuta kila kitu tayari, anajiona mwepesi. Anakukumbatia na kukushukuru kwa sababu anakuona ni mtu wa kipekee. Wengi wamelemaa kwa mfumo dume!
Kufanya hivyo haina maana ya ‘ubushoke’ kama inavyoweza kutafsiriwa, isipokuwa ni njia ya kumpa sababu ya kukupenda. Atakuona ni mwanaume bora uliyekamilika. Usipokuwa naye ataona kuna upungufu mkubwa. Usisome kama mapitio ya vitu rahisi, ila unatakiwa kutunza kichwani na kuhamishia katika vitendo kile ambacho unakipata hapa.
Asilimia kubwa ya watu waliosalitiwa kimapenzi na marafiki zao, ilisababishwa na watu kutoheshimu hisia za wenzi wao. Kiasili, kuna mambo ambayo mtu anakuwa anahitaji kutoka moyoni afanyiwe na mwenzi wake lakini anakuwa hapati, hivyo kusababisha aone pengine jirani anaweza kumtekelezea.
CHUKUA MFANO HUU
Justin na Jamie wapo kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa miaka mitatu sasa. Tatizo kubwa linalowakabili ni kwamba mara kwa mara huwa wanagombana na kusalitiana. Hata hivyo, wao hawajui.
Justin anasema: “Nampenda sana Jamie lakini kuna mambo huwa hanitekelezei, na zaidi huwa nashangaa hata hanionei wivu. Nikiwaona marafiki zangu jinsi wanavyoishi na wapenzi wao, nashangaa kwa nini kwangu haiwi hivyo? Naweza kuwa mbali naye hata kwa siku mbili lakini wala hashtuki, haniulizi.
“Tukikutana haoneshi shauku ya kuwa na mimi mpaka nahisi thamani yangu kwake ni ndogo. Hajawahi hata kunikumbatia na hasemi kama alikuwa amenimisi. Nyumbani kwangu naishi peke yangu lakini hutomsikia akisema anataka kuja mpaka nimuombe, tena kwa kumbembeleza, wakati mwingine anasema yupo bize.
“Tukiwa katika ulingo wa mapenzi haoneshi msisimko. Nijuavyo mimi wanawake wengine hutoa hamasa kwa kuangusha kilio fulani cha mahaba na kusifia jinsi kazi inavyofanyika, Jamie yeye habari hiyo hana. Hata nyonga yake anaibania. Ukimuuliza kama anatosheka anadai anafika bila wasiwasi. Hapa ndipo anaponifanya nijiulize maswali mengi.
“Mara mbili nimejikuta nikitoka na rafiki zake wawili. Wa kwanza alionesha ananijali kuliko hata Jamie mwenyewe. Nilipotoka naye nilijiona mwanaume kamili hasa. Ananiuliza maswali ya mahaba, ananikumbatia kwa bashasha kila tunapokutana. Tukiwa kwenye shughuli ananionesha jinsi anavyoridhika na mimi.
“Mwingine hivyo hivyo, tunapomaliza mchezo ananimwagia sifa kemkemu, ananiambia hajapata mwanaume aliyemsafirisha kule ambako nimempeleka. Katikati ya mahaba, ananililia kwa sauti fulani ya kutoka puani. Itaendelea wiki ijayo.
1 comment:
Haaaa hapo mzee kuna kasehemu kananihusu mimi. Nashukuru kwa kisomo
Post a Comment