ANGALIA LIVE NEWS

Monday, November 24, 2014

NJIA 60 ZA KUMFURAHISHA MUMEO.



Katika mada yangu ya “njia 60 za kumfurahisha mkeo” niliahidi kuendelea na maudhui hii kwa kuwaletea mada ya “kumfurahisha mumeo”. Natangulisha shukrani kwa wale walioniandikia katika E-mail yangu na kupitia WhatsApp. Ifuatayo ni mada husika:

1. Anaporudi kutoka kazini, safarini au kwenye shughuli yoyote iliyowatengenisha, anza kwa salamu nzuri.
2. Unapompokea au kukutana naye basi fanya hivyo ukiwa na uso wa bashasha.
3. Vaa mavazi nadhifu. Jipambe na upake manukato kwa ajili yake.
4. Unapoanza kuzungumza naye anza na mambo au taarifa nzuri, na kama kuna taarifa mbaya subiri mpaka atakapopumzika.
5. Mpokee kwa maneno ya upendo na lugha ya kumpongeza au kumpa pole au lugha yoyote inayoonesha kumhurumia kwa kazi za kutwa nzima.
6. Ipendezeshe na uilainishe sauti yako kwa ajili ya mumeo… usifanye hivyo mbele ya wanaume wengine.
7. Utunze mwili wako na kujiweka katika hali ya umaridadi na siha njema.
8. Oga mara kwa mara, na pia baada ya siku zako.
9. Epuka kuwa katika hali ya uchafu au muonekano mbaya.
10. Epuka mapambo yaliyoharamishwa kama vile kujichora tattoo na kadhalika.
11. Tumia manukato, rangi na mavazi yanayopendelewa na mumeo.

12. Jitahidi mara kwa mara kubadili mtindo wa nywele, manukato na kadhalika. Lakini usizidishe kiwango, na ufanye hivyo kwa mumeo tu au mbele ya mahram wako.

13. Usichelewe kumpa mahaba pindi mumeo anapojiwa na hisia ya kutaka kufanya mapenzi.

14. Mwambie maneno matamu na yenye mvuto wa mahaba.
15. Ridhika na yale uliyoruzukiwa na kukadiriwa na Allah.
16. Kumbuka kuwa utajiri wa kweli hupatikana katika imani na uchamungu.

17. Usihuzunike kwa sababu mumeo ni masikini au anafanya kazi ya kawaida. Watazame maskini, wagonjwa na walemavu kisha umshukuru Allah kwa aliyowajaalia.

18. Usimuombe mumeo mambo mengi yasiyokuwa na ulazima.

19. Uchamungu hauna maana ya kutofurahia mambo mazuri nay a halali, bali una maana ya kuiangalia Akhera na kuyatumia yale uliyojaaliwa na Allah kwa lengo la kuifikia Pepo Yake.

20. Mshajiishe na umhamasishe mumeo kupunguza matumizi na kuweka akiba ya pesa kwa ajili ya sadaka na kuwasaidia maskini na wale wenye dhiki.
21. Kuwa mwenye shukrani kwa mumeo.
22. Ukiwa mwenye shukrani, mumeo atazidi kukupenda na atajitahidi kukufurahisha na kukuridhisha zaidi.

23. Ukiwa mtovu wa shukrani, mumeo atasikitishwa na hali hiyo na kuanza kujiuliza: “Kwa nini nimfanye mambo mazuri mtu asiyekuwa na shukrani?” Epuka hali hiyo.

24. Daima kuwa mtiifu kwake.

25. Shikamana na mumeo, hususan katika nyakati za shida, dhiki, maradhi au mumeo anapofilisika au anapokuwa hana pesa.

26. Muunge mkono kupitia kazi yako, fedha yako au mali yako pindi inapohitajika.
27. Fuata maagizo yake, isipokuwa katika mambo ya haramu. Katika Uislamu, mume ni kiongozi wa familia, na mke ni msaidizi na mshauri wake.

28. Jaribu kuepuka yale yanayomkasirisha.
29. Mfurahishe anapokuwa ameghadhibika.
30. Ukimkosea muombe msamaha.

31. Akikosea usihamaki kwa kumfokea au kuzozana naye. Subiri anapokuwa hana ghadhabu na uzungumze naye kwa amani na kwa kauli nzuri.

32. Akiwa na hasira kutokana na mambo ya nje ya nyumba basi subiri mpaka atakapoondokana na hasira hiyo.

33. Mpe faraja na kumuonea huruma, yumkini akawa amechoka, ana matatizo ya kikazi au kuna mtu kamtusi, n.k.

34. Usimuulize maswali mengi au kung’ang’ania kutaka kujua yaliyotokea. Mathalan, kuna wanawake wengine wakiona mume ana hali tofauti huanza kusema: Niambie kumetokea nini? Lazima utaniambia kilichokufanya mpaka ukawa na hasira hivyo… unaficha nini? Nina haki ya kujua au kuna mwanamke kakuvuruga?

35. Jilinde dhidi ya mahusiano yaliyoharamishwa.

36. Tunza siri za familia, hususan mambo ya chumbani na mambo mengine ambayo mumeo hapendi watu wayajue.

37. Usisahau kushughulikia vizuri malezi ya watoto na huduma za nyumbani. Mumeo atafurahia kula chakula ulichompikia na chenye virutubisho.

38. Zilinde mali na fedha zake.
39. Usiende matembezini au nje ya maeneo ya nyumbani bila idhini yake; unapotoka vaa mavazi sahihi.

40. Usiwakaribishe au kukutana na watu ambao hapendi ukutane nao.
41. Usikae faragha na mwanaume yeyote ambaye sio mahram wako.
42. Kuwa mwema kwa wazazi na ndugu zake. Wakaribishe wageni wake.
43. Jitahidi sana kuepuka migogoro na ndugu zake.
44. Epuka kumuweka katika hali na mazingira ambayo anatakiwa kuchagua kati ya mamaye na mkewe.

45. Onesha ukarimu kwa wageni wake kwa kuwaandalia sehemu nzuri ya kukaa, chakula kizuri n.k.
46. Mhamasishe kuwatembelea ndugu zake nawe uwaalike kuja nyumbani kwako.

47. Wapigie simu wazazi wake na dada zake, watumie ujumbe mbalimbali wa kuwajulia hali, wanunulie zawadi, waunge mkono katika nyakati za matatizo na shida.
48. Usifuatilie au kutengeneza shaka zisizokuwa na msingi.
49. Wivu ni alama ya upendo wa mke kwa mumewe lakini usivuke mipaka ikafikia hatua ukawatukana watu au kuwavunjia heshima.

50. Kuwa mwenye subira na stahmala mnapokuwa katika wakati mgumu kifedha au kimaisha. Kuwa mvumilivu mnapokutwa na majanga mbalimbali na hususan mumeo anapofukuzwa kazi, mpe nguvu.

51. Shirikiana na mumeo na umkumbushe kutekeleza ibada mbalimbali za faradhi na za sunna.

52. Mhamasishe kuswali swala za usiku. Sikiliza na usome Qur’an Tukufu unapokuwa peke yako na ukiwa na mumeo pia. Mdhukuru Allah sana, hususan baada ya swala ya Alfajr na kabla ya Maghrib.

53. Jifunze sheria mbalimbali za Kiislamu na adabu za wanawake.
54. Msaidie mumeo katika kazi zake ikiwa ni pamoja na kumpa nguvu,
kumhamasisha, kumpa ushauri mzuri, kumfariji na kadhalika.

55. Jitahidi nyumba iwe safi, ipanmbe na kuiweka katika mpangilio na mandhari mazuri.

56. Andaa chakula kizuri na kinachojenga afya.
57. Jifunze stadi zote muhimu za kuendesha nyumba kama vile ushonaji, mapishi na kadhalika.

58. Jifunze namna ya kuwalea watoto vizuri na kuwapa mwenendo mwema wa malezi ya kimaanawi.

59. Usitumie fedha zake bila ruhusa yake, hata kama itakuwa kwa ajili ya kutoa sadaka, labda kama una uhakika kwamba ataridhia.

60. Jitahidi kuwaweka watoto katika muonekano mzuri, mavazi safi n.k. Wape chakula chenye virutubisho, zingatia sana afya yao, elimu na maadili mazuri. Wafundishe Uislamu na uwasimulie visa vya mitume na maswahaba.

Ninamuomba Allah azijaze nyumba na nyoyo zetu utuvu, upendo na kuhurumiana sasa na hata milele!!!

Ungana nami katika mada ya “MKE ANAWEZA KUMSHAURI MUME BILA KUMVURUGA AKILI NA KUMUUMIZA”.

Niandikie kupitia: kabuga05@gmail.com au WhatsApp: +255 763 348 213

13 comments:

Anonymous said...

sasa hii ni kwaajili ya waislam tu ama? maana hizo suala ulizo suggest ni kwa ajili ya waislam na siye wakristu ?? try to be general as humu hawaingii waislam tu. thanks

Anonymous said...

naona mwanamke tu ndo anaambiwa afanye haya je mwanamme hakuna la kuambiwa la kufanya.its very wrong ndo maana unakuta kila siku mwanamke yeye kazi yake kumridhisha tu bwana/mume.bwana ghani huyo hasa na mume ajiume na yeye pia.

watoto wa kiume nao wanahitaji wafundwe wajue jinsi ya kuka na mkee si eti leo kila leo mke ndo ayafanye haya yote.

dunia ya leo si ya jana wala ya juzi wanawake wanakwenda mbele nao wanataka kuridhishwa na kuenziwa na kutunzwa.

pesa ya mkee ibaki kuwa ya mkee mume marfuku kugusaaa kama mnataka kwenda na haki za dini na kupika si kazi ya mke kama kweli mnafuata dini.kazi ya mke ni mmoja tu.

watu wamesoma dini wanajua sheria zao usione wanakaa kimya.

Anonymous said...

makala haya mawaidha yake mazuri sana lakini inaonyesha jinsi mwanamkee mwenye nguvu zaidi ya mume,yeye wakumpa moyo,kumburudisha na kuchagia kiakili.
safi sana wanawake daima juu juu zaidi

Anonymous said...

mwanamme bila ya mwanammke anawezaa?hawezi.
mwanamkee bila ya mwanamme anaweza?dio anaweza sema kwenye uzazi tu ndo atahitaji awe na mwanamme

Anonymous said...

Vice versa kwa wanaume. Especially kaka zetu wa kibongo. Ukiwa na mwanamke wako,onyesha unamjali. Siku moja moja nawe mpikie,umpumzishe. Shinda na watoto,mwambie bi. Mkubwa achukue off ,aende shopping,kujipamba n.k. Mkitoka out,then mwaume unatake ur place,serve her drinks,clean up after both of u. Get a chair for her,kama kuna kiti kimoja,then ladies first. Wanaume humweka mwanamke mbele kwanza,that's what a gentleman does.

Unknown said...

Apo unafanya vise vesa mbona maana moja tuu Penye allah weka mungu kwan mungu ni mmoja tu thanls

Unknown said...

Apo unafanya vise vesa mbona maana moja tuu Penye allah weka mungu kwan mungu ni mmoja tu thanls

Unknown said...

Habari naitwa Baby Luna ni mwanamziki kutoka Afrika mashariki nchini Tanzania ningependa kukukaribisha you tube kusubscribe channel yangu bofya link
πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡
https://youtu.be/o9PC8cQKvSk

Unknown said...

Habari naitwa Baby Luna ni mwanamziki kutoka Afrika mashariki nchini Tanzania ningependa kukukaribisha you tube kusubscribe channel yangu bofya link
πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡
https://youtu.be/o9PC8cQKvSk

Unknown said...

Habari naitwa Baby Luna ni mwanamziki kutoka Afrika mashariki nchini Tanzania ningependa kukukaribisha you tube kusubscribe channel yangu bofya link
πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡
https://youtu.be/o9PC8cQKvSk

Anonymous said...

Kumbee ushaelew kwamba Allah ni mungu xx gubu la Nini au ndo imrad ucoment na ww

Anonymous said...

mada ilikuw ndo hyo ukitaka kuhusu wanaume kujali wake zao pia mada zpo gogle acha kicran chako

Anonymous said...

Swadakta