ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, December 3, 2013

KABILA GANI ZURI LA KUOA/KUOLEWA?


NINAWASALIMU kwa jina la Bwana, hasa wakati huu mamilioni ya Wakristo kote duniani wakijiweka sawa kwa kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo wa Nazareti, zaidi ya miaka 2000 iliyopita.

Sijajua kwa nini nimeamua kuandika mada hii, ila nimejikuta tu nikiandika. Lakini nina sababu ambayo nadhani inatosha kukushawishi hata wewe tukajiuliza kwa pamoja. Nimewahi kukutana sana na swali hili na baadhi ya watu wakilizungumzia kwa namna ya kukebehi, kukejeli, kusifu na kuponda baadhi ya makabila linapofika suala la uhusiano wa kimapenzi au maisha ya ndoa.

“Umeoa Mmachame?, umekwisha, hao watu wabaya sana aisee, hawaoni taabu kukuua warithi mali,” mtu mmoja alimshangaa mwenzake baada ya kumwambia kuwa mwanandoa mwenzake anatokea Kilimanjaro katika kabila hilo.

“Hao Wangoni bwana, wape hela watafikisha, lakini mwanamke hafiki aisee, wahuni sana hao,” mwanamke mmoja alimweleza shoga yake baada ya kumtaarifu kwamba anajiandaa kufunga ndoa na mchumba wake ambaye ni Mngoni kutoka Ruvuma.
“Unaishi na Mhaya? Duh, mtawezana kweli, maana hao jamaa wana majivuno?!” mwingine naye anamshangaa mwenzake.

Kwa jumla, katika jamii yetu, tunalo tatizo hili kwa kiwango kikubwa sana, tukibaguana kwa misingi ya dini, kabila, elimu na vitu vingine chungu mzima. Tumeacha kuzungumzia mapenzi kwa maana ya uhusiano, tumeangukia katika kujadili vitu ambavyo havihusiki kabisa.

Rafiki yangu mmoja aliniambia kwamba alilazimika kuomba ushauri kwa watu wazima na majirani, ili aweze kushusha presha ya mama yake ambaye alikataa katakata mpango wake wa kuoa mwanamke anayetokea katika kabila la Warangi, wanaotokea Kondoa mkoani Dodoma, kwa sababu ambazo hazikumtosheleza hata kidogo.

Aliniambia kuwa mama yake alimweleza kuwa wanawake wa kabila hilo ni watu wanaopenda sana kutumia ushirikina katika uhusiano au ndoa zao.

Nimesikia mazungumzo ya namna hii kwa miaka mingi, nimejaribu kuchunguza kwa kuulizauliza watu wa makabila tofauti walio katika uhusiano na hata kusoma baadhi ya tafiti, inaonyesha kuwa hakuna ukweli wowote katika mapenzi yanayohusiana na tabia za kabila.

Hakuna uhusiano wowote kwa mfano, majivuno ya Mhaya na jinsi atakavyoishi kimapenzi na mwanamke ambaye wako kabila tofauti. Ni kweli, kwa nje, inaonekana kama hawa jamaa ni watu wa majivuni, lakini niwe mkweli kuwa ninao marafiki wengi Wahaya, lakini hawana majivuno hata kidogo.

Umalaya, ujivuni, ushirikina, uroho wa mali na vitu vingine, ni tabia binafsi ya mtu. Kulisingizia kabila ni kutotenda haki kwa sababu kwa mfano, wakati tukiambiwa kuwa wanaume wa Kingoni ni watu wa wanawake sana, upo ushahidi wa wazi kwamba Ruvuma si miongoni mwa mikoa yenye kiwango kikubwa cha maambukizi ya gonjwa hatari la Ukimwi!

Mtu anapaswa kufanya uamuzi wa kuingia katika uhusiano wa kimapenzi na mtu kwa kufuata hisia zake na jinsi mwenyewe anavyomchukulia mwenza wake. Kuchagua kabila kama ndicho kigezo cha kuishi katika uhusiano ni ubaguzi, kitu ambacho ni dhambi kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu.

Wengi wameshangazwa na kuimarika kwa uhusiano wao ambao awali ulitiliwa mashaka na watu wengi. Wazee wetu vijijini wangependa tuoe au kuolewa na watu wa kabila letu, lakini katika dunia inayojikusanya kwa kiwango kikubwa na kuwa kijiji, fikra hizi zimepitwa na wakati.

Kitu cha msingi ni kuangalia na kuzifanyia kazi sifa unazozitaka kutoka kwa mpenzi wako. Kama ana upungufu, mchukulie yeye kama yeye na siyo kabila, dini au elimu yake. Mapenzi ni sanaa, ambayo ndani yake haina ukabila, usomi wala imani!

GPL

26 comments:

Anonymous said...

inaonekana unajaribu ku-justfy binti wa ki-nshomire uliyempata. all i can say is good luck!

Anonymous said...

Wasukuma wa Mwanza na Tabora! Wamanyema wa Kigoma!!!!! Hao mwishoooo kamata mmoja utaniambia, si mchezo wajameni!.

naiman64 said...

Ndugu hivi unanishawishi nikaolewe na mkurya kisa ni mapenzi na kila siku tunaona wanawake hawana miguu au mikono kisa mumw kakasirika hapana toa ushawishi mwingine. yanayosemwa yapo japo katika kumi mmoja anakuwa hana sifa hiyo je utamjuaje?

Anonymous said...

Aisee Machame! Wasomi" wako Makini na maisha! Wapambanaji' Si washamba Wa hela! Na wachumi jaribu utajionea mwenyewe!!!

Anonymous said...

tafuta mwanamke wa kisukuma wana upendo sana. my wife of 7 years ni msukuma and I thank God every day kwa kunipa mwanamke mwema kama huyu.

Anonymous said...

Aaaaauw kwelu umenena wachagga tunaheshima saa hatununuriwi kwa chinese wings kama mtaa wa pili! Babu eeeeh kajitafutie kajio kako ka gesi Moshi Tarakea !

Anonymous said...

WAHAYA,WARANGI,WAHEHE,WAMACHAME,WACHAGA, HAYO NI MAKABILA AMBAYO MWANAUME AKIOA KAUMIA KWA UCHAWI, UMALAYA, KUUA WAME ZAO KISA MALI NIVINGINE VNG NI WAKWANZA MAKBILA MAZURI NI WAHA,WASUKUMA, WAFIPA,NA WENGINEO KIDGO BHASI.

Anonymous said...

Kuchagua mtu kwa kuzingatia kabila ni ubaguzi na ni kitu cha kupiga vita! Hiki kitu ndio kinaimaliza nchi yetu na kushindwa kuendelea hata serikali kuacha lugha za makabila kuendelea kuzingumzwa ni kosa na ni miongoni mwa changamoto ambazo wataalamu mbalimbali wameeleza kuwa ni kitu kinachoturudisha nyuma kimaendeleo. Katika nipindi cha Karne ya 8 Uingereza ilikuwa na Makabila 37. Lakini wenzetu waliamua kuwa lugha moja tuu itumike na kupiga marufuku kutumia lunga nyingine! Mwingiliano wao uliwafanya kuwa wamoja na kuendelea. Lakini itashangaa Tanzania bado watu wanajali ukabila. Nchi nyingi za kiafrika hatuendelei kwa kuendekeza ukabila na kudababisha mapigano ya mara kwa mara. Nachoamini ni kuwa utamaduni hubadilika. Hivyo ni vema watu wakazingatia sifa za mtu binafsi bila kuangalia kabila wakati unahitaji kuoa au kuolewa.

Unknown said...

Nawapenda sana warangi

Unknown said...

Naomba ushauli nina mpenzi na nampenda nae anasema ananipenda nifanyaje ili nijue kweli ananipenda na naitaji kweli kuolewa?

Unknown said...

apeleke barua ya posa tu kama anakuenda kweli na unmpenda pia

Unknown said...

Mimi naona kabila zote safi tu kikubwa ni upendo tu

Davis trustworthy media said...

😅😅😅 Sisi wakurya tukaoe wapi jamani

Unknown said...

Jamani vipi kwa majirani zangu wao mnasemaje wadau, wako vizuri kuolew?

Unknown said...

hapo umenena tabia ni ya mtu siyo kabila

Unknown said...

Kwa upande wa wanyamwezi vipi jaman

Anonymous said...

Jamani mim nimempenda mngoni sjui tutawezana ,🤔🤔🤔

Anonymous said...

Kabila gani liko fresh kupata wife

Anonymous said...

Sisi sote ni watoto wa baba mmoja endapo tu makabila tofauti. Cha msingi ni upendo hayo mengine ni mapambio tu

Anonymous said...

Mwisho kufanyaje?

Anonymous said...

Wafipa wako vizuri sana

Anonymous said...

Natafuta binti wa kinyamwezi au msukuma awe umri miaka 28 hadi 35 kwa ajili uchumba mimi nipo dodoma nina miaka 48
0679013627

Anonymous said...

Kaka unaonekana umesoma na elimu yako inafanya Kazi. Barikiwa sana kaka. We need people like these to develop. Asante sana nimesoma nimeelewa nimeipenda

Anonymous said...

Namimi nahitaji kujua upande huu

Anonymous said...

Nipo hapa tafadhali mimi ni mnyamwezi

Anonymous said...

Kwa wafipa hapo umedandanya ndugu