ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, November 9, 2011

KOCHA WA MCHEZO WA NGUMI SUPER D KUDHURIA KOZI YA KIMATAIFA YA NGAZI YA JUU

Na Mwandishi Wetu

KOCHA wa timu ya ngumi ya Ashanti ya Ilala na Mkoa wa Kimchezo Ilala, Rajabu Mhamila 'Super D', ameteuliwa kuhudhuria mafunzo ya ngumi yaliyoandaliwa na Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT) kwa kushirikiana na Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC).

Miongoni mwa makocha wa ngumi watakaoshiriki mafunzo hayo, ni mpiga picha wa Magazeti ya Business Time inayochapicha Magazeti ya Majira, Sports Starehe na jarida la Maisha, Mhamila ambaye maarufu kwa jina la Super D.

Super D mbali na kuwa kocha wa ngumi na mpiga picha, pia ni bondia wa zamani wa ngumi za ridhaa na kulipwa.

Akizungumza Dar es Salaam juzi, Katibu Mkuu wa BFT, Makore Mashaga, alisema kozi hiyo itawahusisha makocha wa mchezo wa ngumi nchini kuanzia Novemba 12, mwaka huu hadi 20, ambapo itafanyika wilayani Kibaha, Pwani.



Mashaga alisema Mkufunzi wa kozi hiyo atatoka nchini Algeria, ameteuliwa na Chama cha Ngumi Ridhaa cha Dunia (AIBA), ambapo makocha  30 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara, wameteuliwa kushiriki.


Mashaga alisema makocha hao wamechaguliwa kwa kuzingatia mchango wao katika ushiriki wa matukio mbalimbali ya BFT, hasa mashindano kwa kuleta timu au mikoa yao kushiriki mashindano mbalimbali yaliyoandaliwa na BFT.

"Baadhi ya makocha hao, walipata  mafunzo ya awali yaliyoandaliwa na BFT, watakaofuzu mafunzo haya, watatambuliwa na kuingizwa katika kumbukumbu za AIBA," alisema Mashaga.

Alisema makocha hao wataweza kufundisha mchezo huo popote duniani na kuruhusiwa kushiriki mashindano yote ya kimataifa kama makocha katika mashindano  yatakayoandaliwa kwa kufuata sheria za AIBA.

Alisema kwa uzoefu wao BFT, wanategemea mara baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo, kutakuwa na ushindani wa uhakika kutoka kwa makocha hao.

Mashaga alisema kwa msingi huo, wanatarajia kupata ushiriki wenye tija katika mashindano kufuzu kushiriki katika mashindano ya Olimpiki 2012, London Uingereza.

nae Super D aliongezea kwa kusema kozi hiyo imekuja wakati muafaka kwa kuwa dhamira yake ni kukuza na kuendeleza mchezo wa ngumi kimataifa Super D ambaye sasa ni muhandaaji wa nafunzo ya ngumi kwa njia ya DVD ambao huwa anaweka matukio mbalimbali ya mapambono ya ngumi za Dunia wakiwemo Floyd Mywherther, Manny Paquaio,Mohamedi Ali, DAvidi Haye, mike Tayson na wengine wengi DVD hizo za mafunzo zinapatikana makutano ya barabara ya Uhuru na Msimbazi au katika kambi ya ngumi ILala na klabu ya AShanti nayo ya ILala.

No comments: