ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, November 15, 2011

Miss Tanzania 2011arejea akitokea Uingereza

Vodacom Miss Tanzania 2011, Salha Izrael akipunga mkono mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana akitokea jijini London Uingereza alikoshiriki shindano la urembo la Dunia Novemba 6,2011.
 Salha Izael akifafanua jambo kwa mwandishi wa Habari na na kando yake ni Mdogo wake
 Mwandishi wa Habari Mwandamizi wa Mwananchi Communication, Majuto Omar akifanya mahojiano na Salha Izrael baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
 Warembo na wanafamilia wakipiga picha ya pamoja na Miss Tanzania 2011, Salha Izrael.
 Warembo Alexia William (kushoto) na Husna Maulid wakiwa na Miss Tanzania 2011, Salha Izarel mara baada ya kumpa mashada ya maua.
Vodacom Miss Tanzania 2011, Salha Izrael (katikati) akiwa na baadhi ya warembo walioshiriki shindano la Miss Tanzania 2011 waliofika kumpokea katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana akitokea jijini London Uingereza alikoshiriki shindano la urembo la Dunia Novemba 6,2011. Warembo hao toka kushoto ni Jenifa Kakolaki, Alexia Willam,Hussna Maulid na Hamisa Hussein.

(Picha kwa hisani ya mrokim.blogspot.com)

No comments: