ANGALIA LIVE NEWS

Monday, November 21, 2011

Mkuu wa ujasusi wa Gaddafi 'akamatwa'-BBC


Aliyekuwa mkuu wa ujasusi katika utawala wa Kanali Gaddafi Abdullah al-Sanussi amekamatwa, serikali ya mpito ya Libya imesema.
Alikamatwa na wapiganaji kusini mwa nchi.
Bwana Sanussi,alikuwa mmoja wa viongozi wakuu katika serikali ya Gaddafi ambaye alikuwa hajulikani alipo.
Mwanawe Gaddafi Saif al-Islam alikamatwa sikuya Jumamosi. Wote,yeye na Bwana Sanussi wanatuhumiwa kwa uhalifu wa kivita na mahakama ya kimataifa ya jinai.

Shemeji ya Gaddafi

Bwana Sanussi, ambaye ni shemeji yake Kanali Gaddafi, inasemekana alikamatwa nyumbani kwa dada yake katika mji wa Sabha ulioko kusini mwa nchi siku ya Jumapili.
Alifahamika kama mtu wa karibu wa marehemu Gaddafi - na mmoja wa watu waliogopewa sana katika utawala huo.
Bwana Sanussi, 62, anatuhumiwa na mahakama ya kimataifa ya jinai kwa kuhusika na ukatili wakati wa kuzima maandamano dhidi ya utawala wa Gaddafi mapema mwaka huu.
Pia ameshutumiwa kwa ukiukaji wa haki za binaadamu, ikiwemo kuhusishwa kwa mauaji ya wafungwa zaidi ya 1,000 katika gereza la Abu Salim mjini Tripoli mwaka 1996.

No comments: