Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa mara nyingine, limetangaza rasmi uuzaji wa nyumba zake mpya linalozijenga katika eneo la Ubungo Flats, lililoko katika makutano ya barabara ya Morogoro na Shekilango jijini Dar es Salaam, kwa bei ya Sh. 67,946,567.86 kwa kila nyumba, bila ya kujumuisha Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT).
Nyumba hizo zipatazo 80, ziko ndani ya majengo manne yenye nyumba 20 kila moja.
Zina ukubwa wa vyumba viwili vya kulala, sebule kubwa inayoingiliana na sehemu ya kulia chakula, jiko la kisasa na zitakuwa ndani ya uzio wa pamoja.
Zinaanza kujengwa Desemba, mwaka huu na zitachukuwa miezi tisa hadi kukamilika kwake. Zinajengwa katika eneo ambalo lina huduma zote muhimu ikiwamo kituo cha afya, shule na maduka.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa NHC, David Shambwe, alisema kwamba mradi huo wa ujenzi utakaogharimu Sh. billioni nne hadi kukamilika kwake ni muendelezo wa uuzaji wa nyumba zinazojengwa na NHC katika sehemu mbalimbali nchini, ikiwa ni kutimiza malengo ya kujenga nyumba 10,000 kwa ajili ya wananchi wenye kipato cha kati na juu na nyumba 5,000 kwa ajili ya watu wenye kipato cha chini.
“Watanzania wanaohitaji kununua nyumba hizi wanapaswa kuchukua fomu kutoka katika ofisi zetu za mikoa zilizopo nchi nzima, ofisi ya mauzo iliyopo pale Ubungo flats, Makao Makuu ya NHC au kwenye tovuti ya shirika” alisema.
Alisema mwombaji atairejesha fomu iliyojazwa na kusainiwa ikiwa na malipo ya awali ya asilimia 10 ya bei ya nyumba kama ushahidi wa dhamira ya mteja ya kununua nyumba na kwamba fedha itakayobakia itatakiwa kulipwa ndani ya siku 90 na endapo muda huo utapita basi, shirika litaigawa nyumba hiyo kwa mnunuzi mwingine.
Shambwe alisema kwamba waombaji wa kununua nyumba hizo wanaweza kwenda benki na kupata mkopo wa nyumba au kulipia moja kwa moja kupitia vyanzo vingine vya mapato alivyo navyo.
Alizitaja Benki ambazo wanunuzi wanaweza kwenda kupata mikopo ya nyumba ni Azania Bank, Bank of Africa Tanzania, Commercial Bank of Africa (cba), Exim Bank, Kenya Commercial Bank (KCB) na National Bank of Commerce (NBC). Nyingine ni National Micro Finance Bank (NMB), Stanbic Bank na twiga Bancorp.
Alisema NHC haiuzi nyumba zilizopo pale Ubungo flats, ila zile inazozijenga.
CHANZO: NIPASHE
Bei haziendani na hali halisi ya maisha ya watanzania; tuwekee picha
ReplyDeleteHizi nyumba zimejengwa kwa ajili ya watanzania wote au za watanzania wenye kipato? Coz mlalahoi ataweza kununua nyumba kwa hy bei? basi si waseme za wakubwa tu?
ReplyDeletebadala ya unit 80 , jenga 160 kwa bei poa , watakuja wenye$$ na watchukua mbilimbili, hakika orodha ya order ya wakubwa tayari, halafu bongo tambarare????
ReplyDelete