MUSWADA wa Sheria ya Mapitio ya Marekebisho ya Katiba wa mwaka 2011, sasa utasomwa bungeni kwa mara ya pili na umetengewa sikutatu za kujadiliwa na baadaye kupitishwa na Bunge.
Tayari hatua hiyo ya Serikali imeshapingwa vikali na wanaharakati na baadhi ya wabunge wakiwamo wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Sheria, Katiba na Utawala ambao wanadai muswada huo unapaswa kusomwa kwa mara ya kwanza kutokana na kufanyiwa marekebisho makubwa tofauti na ule wa awali.
Hata hivyo, jana Waziri wa Katiba na Sheria, Celina Kombani alisema mjini hapa kuwa: “Muswada huu uliposomwa kwa mara ya kwanza haukuondolewa, bali ulipelekwa kwa umma ili ukajadiliwe.”
“Mabadiliko mengi yanayolalamikiwa yalitokana na hoja za wananchi, hii ni ishara kwamba tulizingatia hizo hoja, sasa kwa mujibu wa taratibu za miswada ni kwamba utasomwa kwa mara ya pili, kama mnavyoona kwenye ratiba.”

Mvutano uliokuwapo uliripotiwa kuingia ndani ya Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala na unadaiwa kuwa miongoni mwa sababu za kuchelewa kupangwa kwa ratiba ya Mkutano wa Tano wa Bunge ambayo ilitolewa rasmi jana asubuhi baada ya kuchelewa kwa siku mbili.
Ratiba ya Mkutano wa Tano wa Bunge iliyopatikana jana mjini Dodoma, imeonyesha kuwa muswada huo utasomwa kwa mara ya pili Jumatatu Novemba 14, mwaka huu na kujadiliwa kwa siku tatu mfululizo.
Kwa mujibu wa ratiba hiyo, muswada huo pia utajadiliwa Jumanne, Novemba 15 na Jumatano Novemba, 16 mwaka huu.Hatua ya muswada huo kupangwa kusomwa kwa mara ya pili, inatafsiriwa kuwa ni “ushindi” kwa Serikali dhidi ya waliokuwa wakipinga hatua hiyo kutokana na sababu mbalimbali, kubwa ikiwa ni wananchi kupewa muda zaidi kwa ajili ya kuujadili.
Habari kutoka katika kikao cha kuwapa wabunge mwongozo wa Mkutano wa Tano kilichofanyika jana baada ya Bunge kuahirishwa zinadai kuwa mjadala kuhusu muswada huo umetengewa siku tatu ili kukidhi kiu iliyoonyeshwa na wabunge katika hatua za awali za maandalizi yake.

Kabla ya muswada huo kusomwa kwa mara ya pili na kuanza kujadiliwa, wabunge watahudhuria semina itakayofanyika keshokutwa Jumamosi hatua inayotafsiriwa kuwa ni kujaribu kupunguza hoja ambazo zinaweza kujitokeza na pengine kuukwamisha.
Katika kikao chake cha juzi, Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala ililazimika kuwaita Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Frederick Werema na Waziri Kombani kwenye kikao cha jana ili wafafanue baadhi ya mambo kabla muswada huo haujaingizwa tena bungeni.

Hatua ya muswada huo kusomwa kwa mara ya pili kunaweza kusababisha Serikali kupata wakati mgumu wakati wa mjadala huo wa siku tatu na hata kwenye hatua ya kupitia vifungu vya muswada huo.
Miongoni mwa wanaharakati ambao wanapinga muswada huo kusomwa kwa mara ya pili ni Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na Jukwaa la Katiba ambao wamedai kuwa Waziri Kombani amechakachua muswada huo.Jukwaa hilo lilihoji hatua ya muswada huo kuonekana kusainiwa na Waziri Kombani Machi, mwaka huu na sasa unaelezwa kuwa ni mpya na umekidhi haja kwa ajili ya kusomwa bungeni kwa mara ya pili.
“Haiwezekani watu tunazungumzia muswada mpya, kumbe ulishasainiwa tangu zamani. Hata Aprili tulipomwambia (Waziri) atupe muswada wa Kiswahili, alisema haupo, upo wa Kiingereza tu. Lakini huu umesainiwa Machi 8, 2011. Umetoka wapi? Tungemwelewa kama angeusaini Oktoba 14, mwaka huu,” alikaririwa akisema Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba, Deus Kibamba:
Katika Mkutano wa Nne wa Bunge la Bajeti, wabunge walielezwa kuwa suala la Katiba litaingizwa katika mkutano huu baada ya kupitiwa upya.Mbali na Muswada wa Sheria ya Mapitio ya Marekebisho ya Katiba, Bunge pia litasoma na kujadili Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali za Biashara ya mwaka 2011.
Ratiba hiyo inaonyesha pia kwamba, leo na kesho Serikali itawasilisha Muswada wa Sheria ya Ununuzi wa Umma wa mwaka 2011 ambao utajadiliwa bungeni

Mwananchi
Drama kwa kwenda mbele. MMh !!! Hivi kuna kitu watanzania tunaweza kufanya bila usanii just for the sake ya nchi na kizazi kijacho?
ReplyDelete