Monday, November 7, 2011

Sherehe za siku ya Kuzaliwa Mwanzilishi wa Dini Ya Sikh Guru Nanak

 chakula kilikuwa bure kwa kila mtu
Maelfu ya wafuasi wa dini ya Sikh walijitokeza siku ya Jumapili tarehe 6 Novemba 2011 katika mjini wa Southall, Middlesex UK ili kusherekea siku ya kuzaliwa kwa mwanzilishi wa dini yao Guru Nanak aliezaliwa mwaka 1469 nchini Pakistani.
 Frank akipata chai ya tangawizi na iliki kutoka India
Wakati akiwa na umri wa miaka 30 alipotea kwa hali ya miujiza kwa mda wa siku tatu. Alipo rejea alianza kuhubiri, kufundisha na kuandika dini ya Sikh wakati maisha yake yote. Pia Guru Nanak alisafiri dunia nzima kuitangaza na kujadili dini hii kwa waumini wengine kama waislamu pamoja na Hindus
 Frank akiwa katikati ya mitaa ya Southall kushuhudia sherehe hii
Kwa Miaka zaidi 550 wafuasi wa dini hii wamekua na desturi hii ya kusherekea siku moja kabla ya kuzaliwa kwake Guru Nanak kwa kuandaa maandamano haya makubwa ya Sherehe hii ambayo hufanyika India pamoja na baadhi ya sehemu za nchi ya Uingereza. Kwa kawaida sherehe hizi huongozwa na wafuasi wakuu watano wanaojulikana kama ''Panj Piare'' wakiambatana waimbaji, wanamuziki na timu ya wacheza upanga (Martial Arts) kuelekea hekaluni kwao ''Gurdwara'' Sri Guru Singh Sabha,  hapa Southall hekalu lao ndio kubwa kuliko yote katika bara la ulaya
 halaiki ya kubwa ya waumini wa dini ya Sikh wakisherekea 
Sherehe hizi huanza mapema asubuhi kwa kuimba, kuomba kwa pamoja. Baadae chakula cha kitamaduni kinachojulikana kama''Langar'' hutolewa bure kwa kila mtu.
 Hata watoto nao walikuja kusaidia kutayarisha chakula

Maandamano yakiendelea 
 Muasisi wa Dini ya Sikh Guru Nanak
 Southall Palikuwa hapatoshi.
 wadau wakiwa kazini kutayarisha chakula
 wakati wa kupata mapocho pocho
Waumini wa dini ya Sikh wakiazimisha siku hii

Maandamano ya Southall yanaitwa Nagar Kirtan,
Asanteni,
URBAN PULSE CREATIVE

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake