ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, November 9, 2011

Tevez akwepa mazoezi Manchester City-BBC

Tevez akwepa mazoezi na kwenda kwao Argentina

Carlos Tevez ameshindwa kufika mazoezini katika klabu yake ya Manchester City siku ya Jumatano asubuhi

Manchester City walitazamia mshambuliaji huyo angekuwepo mazoezini kwenye uwanja wa mazoezi wa Carrington, licha ya kuonekana kwenye picha akiwasili Argentina siku ya Jumanne.
Alisafiri kuelekea Amerika Kusini katika siku ambayo iliarifiwa asingepinga mashtaka yaliyomkabili kuhusiana na mechi dhidi ya Bayern Munich.
Tevez huenda sasa akakabiliwa na hatua kali zaidi za nidhamu kutokana na kukwepa mazoezi.

Wachezaji wengi wa Manchester City kwa sasa wapo nje kwa ajili ya timu zao za taifa lakini Tevez, ambaye hajacheza soka tangu Manchester City ilipoilaza Birmingham mabao 2-0 mwezi wa Septemba, alitakiwa kubakia Manchester kuendelea na mazoezi ya peke yake.
Mshambuliaji huyo hayumo katika kikosi cha Argentina kitakachopambana dhidi ya Bolivia na Colombia, wiki ijayo.
Siku ya Jumanne ilikuwa ya mapumziko, lakini Tevez alitazamiwa kurejea mazoezini Jumatano asubuhi.
Na baada ya mteja wake kuonekana katika picha nchini Argentina, msemaji wa mchezaji huyo, Paul McCarthy, alisema: "Amekwenda kuangalia familia yake.
City ilimtia hatiani mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester United kwa kukiuka mambo matano katika mkataba wake wakati alipokataa kucheza mechi ya Ubingwa wa Ulaya dhidi ya Bayern mwezi wa Septemba.
Meneja Roberto Mancini alitaka kumuingiza Tevez zikiwa zimesalia dakika 35 kabla mchezo kumalizika lakini aligoma kupiga jaramba.
Alisimamishwa mara moja kwa wiki mbili na kukatwa mshahara wa wiki nne, adhabu ambayo ikapunguzwa kuwa mshahara wa wiki mbili baada ya Chama cha Wacheza Soka wa Kulipwa kuingilia kati.
Baada ya muda wa mwisho wa kukata rufaa kupita siku ya Jumanne, ilionekana kwamba Tevez ameimarisha uhusiano wake na klabu hali itakayomfanya aondoke katika timu hiyo vizuri, iwe kwa mkopo au moja kwa moja itakapofika mwezi wa Januari.
Inaaminika Tevez anaona akiondoka moja kwa moja katika klabu ya Manchester City itakuwa nafuu zaidi kwake.

No comments: