Tuesday, November 15, 2011

TUNAWASUBIRI MAHUJAJI

 Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam na mikoa jirani ambao ni waumini wa Dini ya Kiisalamu wakiwa wameweka kambi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam wakiwasubiri ndugu, jamaa na marafiki zao ambao walienda kufanya ibada ya Hija inayofanyika kila mwaka nchini Saudi Arabia. Mwaka huu siku kuu ya Id El Haji ilisheherekewa Novemba 6, 2011. Maelfu ya Waumini wa dini ya Kiislamu wake kwa waume walisafiri kwenda nchini Saudia katika Ardhi ya Makka ambayo ni ardhi ya Wahyi,kushiriki katika Ibada hiyo. 
(Picha kwa hisani ya mrokim.blogspot.com)

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake