Thursday, November 10, 2011

UZURI HAUKUSAIDII KITU KAMA HUJUI 'MAJAMBOZI'


Ni wiki nyingine tena tunakutana kupitia safu hii nikiamini umzima na unaendelea vyema na majukumu yako ya kilasiku kama kawaida.

Mimi mzima na bado naendelea kuzungumzia mapenzi, mapenzi haya haya ambayo yamekuwa yakiwaliza baadhi ya watu kila kukicha.

Wapo wanaojuta kupenda lakini mbaya zaidi wapo wanaolia kwa sababu ya vitu vidogo vidogo ambavyo vimekuwa haviwaendei sawa katika uhusiano wao. 

Ni jambo lililo wazi kwamba, usaliti umekuwa ukiwatesa wengi tena ukijaribu kuchunguza sababu za baadhi ya watu kuwasaliti wapenzi wao, kutoyajua mapenzi yale ya faragha ni moja wapo.

Inakuwaje?

Wapo wasichana au niseme wanawake ambao kimaumbile wana mvuto sana. Wamejaaliwa uzuri wa sura na kila kitu kiasi cha kutamaniwa na kila mwanaume wanayekutana naye.

Lakini linapozungumziwa suala la mapenzi kwa mwanamke, wanaume wanaangalia vitu vingi, achilia mbali hilo la muonenako, pia wanaangalia  utundu na ubunifu wa faragha. Hapo ndipo panapowakosesha raha baadhi ya wanawake wazuri.

Wanakuwa ni wenye kupata bahati ya kupendwa lakini hao hao ndiyo wale ambao kila siku wanaachwa. Si jambo la ajabu huko mtaani kukutana na msichana mkali ile mbaya lakini akawa si mtu wa kutulia na mwanaume kwa muda mrefu, kwanini? Kwa sababu hayajui mapenzi.

Ni tatizo siriasi?
  
Msichana mzuri aliyeumbika kutoyajua majamboz ni tatizo na ndiyo maana anaweza kuwa mtu wa kulia kila siku. 

Anaweza kukumbana na malalamiko kutoka kwa mpenzi wake kwamba anachokipata ni tofauti na alivyotarajia. Hakuna kinachowauma walio wengi kama kusikia kutoka kwa wapenzi wao kuwa hawawaridhishi.

Kwa maana hiyo ni tatizo siriasi lakini lina ufumbuzi wake. Hakuna aliyezaliwa na kuanza kutembea moja kwa moja, vile vile  kuingia kwenye uhusiano ukawa hujui lolote siyo tatizo ila unachotakiwa kukifanya ni kujifunza.

Zungumza na wataalam wa masuala ya mapenzi, soma vijarida na magazeti, naamini utapata elimu tosha ya kuweza kumfanyia mpenzi wako yale yatakayomfurahisha.

Ugoigoi faragha kwa mwanamke ni chanzo cha wengi kusatiliwa, tena utasalitiwa zaidi kama kila siku utakuwa ni mtu yule yule, yaani hujifunzi chochote. Mwanamke lazima awe mbunifu kwa mpenzi wake, abuni mbinu za kumdatisha ili kuhakikisha haachwi kirahisi.

Unapobaki kujisifia kuwa wewe ni mzuri wakati huna mashamsham yoyote itakuwa ni kazi bure. Matokeo yake sasa utashangaa mpenzi wako anakwenda kwa mwingine ambaye ukimuangalia na kujilinganisha na wewe, unaanza kujiuliza, hivi alichokifuata kwa yule ni nini?

Hakuna kingine, kafuata majamboz. Ndiyo maana nikasema, uzuri wako kama hujui chochote faragha, ujiandae kusalitiwa kila siku na mwisho wake utaachwa.

Ni majamboz tu?

Sifa za mwanamke anayeweza kutulia kwenye uhusiano ukiachilia mbali uzuri wa sura na umbo, tabia njema nalo ni jambo la msingi. Kama umzuri, unayajua mambo ya chumbani ile mbaya ila huna tabia njema, ni tatizo. Waswahili wanasema, tabia njema ni silaha. 

Ushauri wangu

Ili uyafurahie maisha yako ya kimapenzi, hakikisha unakuwa imara kila idara. Kwanza mpende mpenzi wako kwa maana halisi ya kumpenda halafu jitahidi kumpatia furaha ya kweli.

Miongoni mwa mambo yanayoweza kumfurahisha mpenzi wako ni kumshibisha pale mnapopeana chakula cha usiku, ale ashibe na wewe ushibe, mtadumu.

Mbinu za kumshibisha mpenzi wako, zipo nyingi ila kwa kuwa ukurasa huu unasomwa na watu wa kila rika, siwezi kuandika. Hata hivyo, unayo nafasi ya kuwasiliana na mimi kupitia namba zangu hapo chini ili nikupe muongozo katika hili.

Tukutane tena wiki ijayo.


chanzo:www.globalpublishers.info

2 comments:

  1. Aaaah mbona unaonea wanawake tu hta hao wanaume wapo ambao hawawajibiki vilevile na midomo yao michafu kama nini na kupenda kufanya majambozi na kila mwanamke,kuna wanaume anakwamia unajua kila kitu ila ukitakaa uwe juu lazima uluke ukuta sasa hiyo si balaa jamani na mungu hakupi vyote hapo kwangu tabia #1majambosi2,ubunifu3 kama hivyo humu wanasoma watu wa kila rika, niambie nikupostie coment zangu?

    ReplyDelete

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake