Bw. Shaban Abdallay |
KIJANA Shabani Abdallay (26) Mkazi wa Gongo la Mboto Mzambalauni amewaomba wafadhiri na viongozi mbalimbali kujitokeza
kumsaidia kwa kumpatia mtaji wa kuuza vocha kutokana na ugonjwa wa tende la nguu alionao ambao hawezi kufanya kazi yoyote.
Akizungumza mara baada ya kufika kwenye Ofisi za majira zilizopo mtaa wa
Lugoda Dar es Salaam jana, Abdallay alisema kuwa tatizo la mguu huo ni moja ya sababu kubwa ambayo imekuwa ikimsababisha kutofanya kazi yoyote hivyo kuwa tegemezi kwa ndugu na jamaa.
Alisema kuwa siyo ndugu wote wenye moyo wa huruma, hivyo kusababisha ndugu wengine kumuona ni kero na ndio maana aliamua kufika kwenye ofisi hizi kwa ajili ya kuomba msaada kwa mtu yeyote ili aweze kujishughulisha na badaye kupata kipato cha kuweza kujikimu kwenye maisha yake.
Alisema kuwa pamoja na msaada huo wa kuuza vocha vile vile anaomba ikiwa anaweza kujitokeza mfadhiri ambaye anaweza kumsaidia kupata matibabu ya kuwa akiudhuria kriniki ndani ya miaka mitatu ili mguu huo uweze kunywea.
"Mguu huu ulianza kuvimba taratibu tangu mwaka 2000, nimezunguka katika mahospitali mbalimbali ikiwamo, Ocean Road, Amana, Hospitali ya Tumbi Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na nyingine nyingi lakini nilipoenda katika Hospitali ya Macho ya CCBRT walinieleza kwamba Tende haiwezi kupona badala yake nitumie dawa kwa muda wa miaka mitatu ili kuweza kupunguza maumivu na homa kali ninayoipata lakini mguu hauwezi kunywea," na kuongeza
"Hivyo basi baada ya kupata majibu ya kukatisha tamaa nikaamua nikae nyumbani lakini naona ninavyozidi kukaa umri unaenda, hivyo inaweza kufikia mahari nikakosa kabisa mtu wa kunisaidia lakini nikipatiwa mtaji nitaweza kujikwamua na kuondokana na hali ya kuwa ombaomba," alisema Abdallay.
Aidha alisema kuwa pamoja na kuomba mtaji huo lakini kama kuna uwezekano wa matibabu anaomba mfadhiri yeyote kujitokeza kwani amekuwa akisumbuliwa na homa za mara kwa mara pamoja na maumivu makali kwenye mguu huo uliovimba.
Hata hivyo alisema kuwa hali ya maisha yake kuwa magumu pia imechangiwa zaidi na kufariki kwa wazazi wake na kusema kwamba marehemu mama yake ambaye alikuwa akimsaidia alifariki mwaka 2006 wakati baba yake alifariki mwaka 2009.
MAJIRA
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake