ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, November 16, 2011

Watanzania wenzangu Nchini Marekani tunaombwa tuchangie Mchango wa Mazishi ya ndugu yetu Nassib Manyala

Nassib Manyala Enzi ya Uhai wake

Ndugu Watanzania,
Siku za nyuma tuliwatangazia kifo cha Ndugu yetu  Nasibu Juma Manyala
kilichotokea  huko Michigan.Tayari Powers of Attorney ambayo ilikuwa
ikisubiriwa ili taratibu nyingine ziweze kukamilika, imekwishatolewa na
Familia, kwa Professor Deo Ngonyani wa Michigani ili aweze  kusimamia
mazishi kwa taratibu za Kiislamu.
Mazishi yatafanyika siku ya Ijumanne tarehe 22.11.2011 huko huko Lancing
Michigan.
Ili kufanikisha mazishi haya ya Ndugu yetu,tunaombwa kutoa michango yetu
ya hali na mali.Unaweza kutuma fedha kupitia:
Nasibu Juma Manyala(Memorial Account)
MSU Federal Credit Union,
Memorial Acc#43380705 Routing#272479663
Au unaweza kuwakabidhi wafuatao:
1.Professor Deo Ngonyani-Simu 517-614-3543
2.Mussa Maingu-Simu 517-980-4444
3.Abbas Missana-Simu 202378-8066
4.Dj Luke Joe-Simu 301-661-6696
Asanteni

No comments: