ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, January 29, 2012

TWIGA YAIBANJUA NAMIBIA 5-2

 Mshambuliaji wa Twiga Stars, Mwanahamis Omari 'Gaucho', mfungaji pekee wa mabao 2 kati ya 5 ya Twiga, akijiandaa kupiga shuti, wakati wa mchezo wa kutafuta kufuzu kwa fainali za Afrika kwa Wanawake, zinazotarajia kufanyika mwezi Juni mwaka huu.
Mchezo huo umemalizika muda mchache katika uwanja wa Taifa.

Mabao ya Twiga yalifungwa na Mwnahamisi Omar katika dakika 21, Asha Rashid 'Mwalala', bao la pili dakika  46, bao la tatu Etoe Mlenzi, dakika ya 84, Asha Rashid,bao la nne dakika ya 88, na bao la tano, likifungwa tena na Mwanahamis, dakika ya 90+. Mabao ya Namibia mawili ya yamefungwa na Beki wa Twiga, Etoe, aliyejifunga dakika ya 29 na bao la pili likifungwa na Juliana Skrywer, dakika 73.

Kwa matokeo hayo sasa Twiga Stars inatarajia kukutana na mshindi kati ya Misri au Ethiopia ambapo Misri ilikuwa inaongoza kwa mabao 4-2 dhidi ya Ethiopia. 
 Mshambuliaji wa Twiga, Asha Rashid, akiwatoka mabeki wa Namibia.
 Kiungo wa Twiga, Fatuma Mustafa, akiwatoka mabeki wa Namibia.
 Sehemu ya mashabiki waliojitokeza kuishangilia Twiga Stars, wakiwa na mabango yenye ujumbe wa kuhamasisha timu hiyo.
 Mwanadada akionyesha uwezo wake wa kuchezea mpira wakati wa mapumziko.
 Mwanadada huyo, akiendelea kufanya vitu vyake uwanjani na kuwafurahisha mashabiki.
Wachezaji wa Twiga, wakimpongeza mwenzao, Mwanahamis Omar, kwa kazi nzuri aliyoifanya katika mchezo huo.

Picha kwa hisani ya Sufiani Mafoto Blog

No comments: