Monday, February 27, 2012

Kalusha Bwalya: Msione hivi, tulijiandaa tangu 2006

LUSAKA, Zambia
RAIS wa Chama cha Soka Zambia, FAZ, Kalusha Bwalya amesema hakuna njia ya mkato kutwaa ubingwa wa Afrika (AFCON).
 
Kalusha anasema Zambia ambayo haijawahi kutwaa ubingwa wa AFCON mafanikio yake yamekuja baada ya maandalizi ya muda mrefu, tangu 2006 mara baada ya Chipolopolo kushindwa kufuzu kwa Fainali za Kombe la Dunia la FIFA.
 
Akiandika kwenye kolamu yake kwenye mtandao wa FAZ, Kalusha anasema kuwa FAZ imejiweka kwenye mstari, na furaha zaidi kuona matunda yake yamepatikna.
 
Anasema, mja ya hazina kubwa iliyoibeba Chipolopolo ni umoja, uzalendo na mshikamano walio nao wachezaji kitu ambacho mataifa mengi makubwa ya soka Afrika yanakosa.
 
Kalusha anasema kila mchezaji anafahamu uzuri na udhaifu wa mchezaji mwingine na hiyo nio kutokana na kutengeneza kikosi cha muda mrefu bila kubadilishabadilisha wachezaji.
 
Anasema wakati Zambia haina wachezaji wenye majina makubw awanaocheza Ulaya, walicheza kitimu, na hiyo ilijidhihirisha katika Fainali za  2012 AFCON.
 
"Hakuna njia ya mkato kushinda taji kubwa kama hili la (AFCON). Kama wewe ni timu ndogo, lazima utapanda kati ya mataifa yenye majina makubwa lakini kama unataka mafanikio, utakuwa na uwezo wa kucheza na kila timu.
 
"Na hich ndicho tulichokifanya. Mafanikio haya ni mipango ya muda mrefu, tulisonga mbele baada ya kushindwa kufuzu kwa Kombe la Dunia 2006.
 
"Unawza kuwa na kikosi cha wachezaji wote wakali lakini kama hawachezi kitimu, hawawezi kushinda. Umoja wetu ndicho kilichotufanya tupate mafanikio haya," anasema mchezaji bora wa Afrika 1988.
 
Kalusha anasema Zambia imebarikiwa kuwa na kocha bora, Herve Renard, ambaye anaheshimika kwa wachezaji lakini pia hamuonei mtu haya hata kama hana nidhamu.
 
Wachezaji wanamuamini kwa tekniki na taktiki.
 
Nahodha huyo wa zamani wa Chipolopolo anasema Zambia iliingia katika Fainali za AFCON mwaka huu wakiwa na matumaini na morari na pamoja na hayo hakuna hata mmoja aliyeipa Zambia nafasi.
 
"Of course, imekuwa kama faraja kwani tumetwaa ubingwa kilomita chache ambako wachezaji wetu 23 walifariki katika ajali ya ndege miaka 19 iliyopita," anasema Kalusha, ambaye alinusurika katika ajali hiyo na kuamua kwenda moja kwa moja Senegal kwa ajili ya mechi hiyo ya 1994.

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake