
Mkuu wa Gereza la Mahabusu mjini Songea,SP Sylvester Shija (kushoto) kwa niaba ya Amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama nchini Rais Jakaya Kikwete,akimvalisha cheo staff sajent Anna Alexander wakati wa hafla ya kuwapandisha vyeo askari wa nne wa Jeshi hilo Mjini Songea leo.

Baadhi ya asakari magereza kutoka gereza la mahabusu mjini Songea wakiwapongeza askari wenzao wanne walipandishwa vyeo kwa ngazi mbalimbali mjini songea leo.

Mkuu wa Gereza la Mahabusu Mjini Songea,SP Silvester Shija akizungumza na askari pamoja na maofisa wa jeshi hilo mkoani Ruvuma mara baada ya kuwapandisha vyeo askari wa nne kutoka koplo hadi sajent na wengine kutoka sajent hadi staff sajent, kwa niaba ya Amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama hapa nchini Rais Jakaya Kikwete.hafla hiyo imefanyika leo mjini humo.Picha na Muhidin Amri
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake