Akimudu vilivyo gitaa la Solo
Akipapasa Kinanda
Asha Baraka akimfurahia Nape wakati akifanya vitu vyake
Hapa akionyesha mautundu katika Tumba, pembeni yake ni Victor Nkambi na Msafiri Diouf
Kija akimwangalia kwa makini Nape akipiga gitaa la Bass!
Nape Nnauye akipiga Drums huku Msafiri Diouf akiimba
Salam,
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Nape Nnauye leo alipata fursa ya kipekee kujiunga na Bendi ya Twanga Pepeta "Kisima Cha Buruduni" na kufanya nao mazoezi ndani ya ofisi za Aset. Baada ya kufanya makamuzi ya nguvu ilidhihirika wazi kwamba ukiachilia mbali siasa Nape ni msanii mkali wa kuimba, na kupiga vyombo mbalimbali vya muziki. Aidha Mkurugenzi wa Aset Asha Baraka alifurahishwa na kumshukuru sana Nape kuja kuwatembelea na kuwapa sapoti, vilevile alimuahidi kuwa nafasi yake itakua wazi kwenye bendi mara tu atakapo amua kuachia ngazi kutoka katika jukwaa la siasa na kuamua kujiunga katika tasnia ya muziki.
Asanteni.






No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake