Pointi kwamba lazima furaha itimizwe na pande zote mbili ndiyo ilinifungia sehemu ya nne ya makala haya. Vizuri kukumbuka kile ambacho nilikiandika kwa sababu yapo mengi niliyoyafafanua kwa undani kwa lengo kupanuana ufahamu wa masuala ya mapenzi.
Nasisitiza kuwa lazima kila mmoja ajitume kugharamia furaha ya mwenzake, vinginevyo itakuwa ni sawa na kucheza kombolela. Wewe unalinda kopo, mwenzako anakuja kulibutua.
USIJARIBU MAPENZI
Hiki ni kipengele kingine cha
katiba. Dhana ya mapenzi duniani kote inaelekeza kwamba asili yake ni moyoni. Hii ina mantiki kuwa ndani ya kila mtu kuna vitu ambavyo anahisi kuhitaji mwenzi wake awe navyo. Sura, umbo na tabia.Hiki ni kipengele kingine cha
Hata hivyo, kuna nakshi nyingi ambazo si za lazima lakini hutokea kuwavutia watu na kufunika hata yale ya msingi. USHAURI: Zingatia sifa muhimu na kuachana na vionjo vya ziada (accessories).
Kuna mwanamke yeye huvutiwa na mwanaume mwenye kucha ndefu. Ukimuuliza, anakwamba basi tu napenda. Mwingine anaweza kusema: “Nikiwa naye napenda kuichezea, naskia raha!” Yupo atakayekueleza: “Ile kucha yake akinipitishia mgoni au shingoni kwangu taabani!”
Ni vionjo tu vya ziada! Kuna wasiotaka mambo mengi ila wakikutana na watu ambao wananukia ni balaa! Wapo watakaosema wanataka wachangamfu, ingawa mapepe yakizidi nayo ni tatizo kubwa, ila mwingine atadai anahitaji mpenzi anayejua Kiingereza.
Ipo sifa nyeti kwenye dimbwi la mahaba. Kama karata zako unazicheza vizuri kwa mwandani wako na kuhakikisha kila mnapoachiana anakuwa ameridhika kwa 100% ni turufu ya kulinda penzi lako.
MAWASILIANO
Ni nguzo kuu ya uhusiano. Ikiimarishwa huchochea amani ya kudumu lakini kinyume chake ni kichocheo cha wapenzi kuachana. Ni vizuri kujifunza lugha inayoweza kukufanya uelewane na mwenzako. Sauti yako ukiwa mtaani itofautiane na ile ambayo unaitumia chumbani.

Pengine una kawaida ya kutoa majibu ya mkato unapokuwa unazungumza na rafiki zako, lakini tabia hiyo hutakiwi kuizoea pale unapokuwa na mwenzio chumbani. Ikiwa umezoea kuwaita wenzako: “Wewe!” Mwenzi wako hutakiwi kumwita hivyo.
Ni elimu ambayo kila mtu anatakiwa kuwa nayo kwamba kutofautisha maeneo ni jambo la busara. Kwamba sura yako iwe nyingine unapokutana na watu wa mitaani, itofautiane unapokuwa na wazazi, vivyo hivyo pale ambapo upo sehemu ‘spesho’ na mwenzi wako.
Lazima uwe unabadilika kama kinyonga. Ukiwa kazini mbele ya watu unaowaongoza unazungumza kwa sauti ya amri, lakini hiyo hupaswi kuitumia unapokuwa na wazazi wako. Unaongea kwa sauti kali ya kuamrisha mbele ya baba yako, hiyo adabu umefundishwa wapi?
Kuna lugha ya kuzungumza ukiwa na mwenzi wako. Ni mwiko kutoa sauti ya kuamrisha. Ni vizuri kumnyenyekea lakini si katika kiwango ambacho kitakufanya uonekane una kasoro za kisaikolojia. Tawile kwa kila linalosemwa na mpenzi wako hairuhusiwi, unatakiwa kuweka mbele hisia zako.
Upole kupitiliza hauna maana kwamba wewe ni mpenzi sahihi. Eti, utaonekana una nidhamu na unamsikiliza vizuri mwenzio, la hasha! Utatambulika kuwa mtu hai kulingana na jinsi akili yako inavyofanya kazi. Namna hisia zako zinavyoonesha uhai unapogushwa na matukio mbalimbali ndivyo na ubinadamu wako unavyosomeka.
Unahoji mambo kwa sauti yenye ujazo wa kutosha, unachukia pale unapoona mambo hayajaenda sawa, unaumia pale unapotendwa na unafurahi mipango inapokuwa chanya. Hii ndiyo mantiki ya kukutaka uwe na akili hai. Itashangaza umepata habari kwamba mwenzi wako yupo gesti na mpenzi mwingine halafu utabasamu.
Sumu hatari inayosababisha mmomonyoko wa ndoa au uhusiano wa kimapenzi kwa watu wengi ni kushindwa kujipanga kimaeneo. Ratiba za ofisini kuingiza nyumbani. Marafiki kuathiri taratibu za mapenzi yenu, ingawa kila kitu kina umuhimu wake kulingana na wakati husika.

Umeudhiwa na wafanyakazi wenzako kazini, unatakiwa kuweka hekima mbele. Unarudi nyumbani ukiwa na imani kwamba huko utakutana na mwenzi wako na ndiye mfariji wako. Kichwa kizito, basi mueleze mwenzio ajue kinachokusibu kuliko kumpa majibu ya mkato. Itakuharibia badala ya kukusaidia
Ninachosisitiza hapa ni kuwa uhusiano wa aina yoyote unadumishwa na mawasiliano. Lugha yako mbele ya mwenzi wako ina nafasi kubwa ya kukufanya uendelee kufurahia penzi lake. Kinyume chake unaweza kujikuta ni kero kwake. Atakuvumilia mwisho atachoka kwa sababu hujui kubembeleza, unapenda kuamrisha.
www.globalpublishers.info
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake