Tuesday, March 20, 2012

Wanafunzi 234 waliofaulu darasa saba wahawajui kusoma, kuandika

 
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo 
Wanafunzi 234 kati ya waliofaulu mtihani wa darasa la saba mwaka jana, na kuchaguliwa kujiunga na  kidato cha kwanza mkoani Mbeya hawajui kusoma wala kuandika.

Akizungumza na NIPASHE jana ofisini kwake, Jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo, alisema wanafunzi hao wamegundulika baada ya kufanyiwa mtihani wa majaribio.


Alisema aliagiza maofisa elimu nchini kuhakikisha wanafunzi wanaojiunga na shule zote za sekondari wanafanya mtihani wa majaribio. Mitihani huo ulifanyika kuanzia Februari 28, mwaka huu, baada ya kubaini kuwapo udanyanyifu.
Alisema Mkoa wa Mbeya hadi jana ndio walianza kutuma taarifa za mitihani hiyo wizarani na kwamba anasubiri mikoa mingine kutuma. Alisema wakishapata mikoa hiyo wanafunzi watarudishwa nyumbani.
Alisema  wizara imeunda tume ya kutembelea shule zote nchini, kuanzia Aprili Mosi ili kutafuta ukubwa wa tatizo hilo kisha watakaa kama kamati kulijadili na kwamba, walimu watakaobainika walihusika katika udanganyifu huo wa mitihani  watawajibishwa.
Mwaka jana katika mtihani wa kumaliza darasa la saba, kulikuwapo na udanganyifu mkubwa katika mitihani na kufanya wanafunzi wengi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kujikuta hawajui kusoma wala kuandika.
Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka jana, ni 43,240 wavulana wakiwa 21,104 na wasichana 22,104.
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake