Mh Balozi Kallaghe Akitoa hotuba juu ya Muungano
Mh Balozi na Mama Balozi wakifungua Mziki
Mh Naibu Balozi Kilumanga akicheza na Mchumba wake Irene
wadau wakiruka majoka
Wakati wa cheers .
Salam,
Urban Pulse na Miss Jestina Blog wanakuleta taswira ya sherehe za muungano wa Tanganyika na Zanzibar iliyofanyika hapa Tottenham, london Jumamosi tarehe 28.4.12.
Sherehe hii ilihudhuriwa na wadau mbalimbali, Mgeni rasmi alikuwa balozi wetu Mh Peter Allan Kallaghe akifuatana na mkewe, Naibu balozi pamoja na baadhi ya maofisa wa Ubalozi wetu hapa jijini London.
Aidha wakati akitoa hotuba yake Mh Balozi Kallaghe ailiwashukuru wadau na watanzanzia wote waliojitokeza leo kuja kuadhimisha sherehe hii na kuwasihi kuendeleza kudumisha muungano wetu uliodumu kwa miaka 48 sasa. Pia aliwaomba wadau wote kuendelea kufuatilia mchakato mzima wa kutafuta katiba mpya ya nchi yetu unaondelea nyumbani.
Kwa picha zaidi za matukio bofya hapo chini
Sherehe hii iliandakiwa na Swift Freights UK pamoja na Pit Stop '' Uwanja wa Nyumbani''
Asanteni,
Urban Pulse na Miss Jestina Blog
No comments:
Post a Comment