Advertisements

Monday, April 23, 2012

Elizabeth Michael ' Lulu' Alipotinga Mahakama Ya Hakimu Mkazi Kisutu Leo,Kesi Kusikilizwa tena Mei 7


Mshatkiwa Elizabeth Michael |(17), ' Lulu'  akielekea kupanda ngazi na kupandishwa Kizimbani Kesi hiyo  ilikuja kwa ajili ya kutajwa  Upelelezi haujakamilika hiyo ni kwa mujibu wa Wakili wa Serikali Elizabeth Kaganda alisema mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Rita Tarimo  hivyo kesi hiyo  itatajwa tena Mei 7 mwaka huu. Mtuhumiwa amerudishwa rumande.
 Akizindikizwa ndani ya chumba cha Mahakama ya hakimu mkazi kisutu jijini Dar es Salaam leo
Mshtakiwa akipanda ngazi kuelekea Kizimbani ambalo kesi yake ilitajwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam huku akiwa katika ulinzi mkali kutoka kwa askari  Magereza.Picha na Mdau Khadija Kalili (Picha kwa hisani ya Haki Ngowi)

5 comments:

Anonymous said...

Pole elizabeth hata utoke jela mshkaji utanyooshewa vidole sana iliyobaki tafuta tu mume uolewe utulie labda uhame dar itasaidia sana manake kama huku ulaya kazi kupata ingekuwa tabu sana na rekodi yako ndio ingekuwa tayari imeharibika, lakini ngoja tusikie ilikuwaje manake wakati wewe ni mpenzi wake SK mwenzio kajitokeza na mtoto.

RIP SK

Anonymous said...

Huyu mtoto anasikitisha saaana, from uraiani kwenye chips kuku, to sero kwenye kulala na kunguni,mikojo , haja kubwa, chawa, harufu ,kulala sakafuni , kula ugali na maharage yaliyooza, kutembea peku ktk uchafu humo ndani, sio mchezo jamani,
iwe kahusika au hajahusika anaumia sana,
na pia akikumbuka tu kuna roho imepotea na yeye anahusishwa sio kitu kidogo kabisa.
yani namsikitikia sana ila namuombea Mungu ampe nguvu,na haki itendeke iwe ana kosa au hana.
mdada wa DC

Anonymous said...

did she real need all these police magereza kumpeleka mahakamani? Watanzania tuna shughuli. Hao wote wangebaki kazini wafanye kazi. This is so sad.

Anonymous said...

Hao Mapolisi NI kwausalama wake au siyo wananchi wanaweza wakamuuwa.

Anonymous said...

This is sooooo crazy,Tanzania wake up and use your head did u think this 18yrs old girl killed Kanumba?Its Impossible,Kanumba alifariki siku yake ilikuwa imeshafika kila mtu duniani ana siku yake ambapo Nobody knows ni when.Please msimuumize mtoto wa watu hana kosa lolote,I hope mahakama itachunguza zaidi na kuona she is Innocent.Lulu mimi niko na wewe na Mungu pekee ndiye atakaye kupa nguvu na kukulinda this is totally crazy,hajamzika mpenzi wake,hajaomboleza kifo cha mpenzi wake,hajaona kaburi la mpenzi wake.Hivi nyie watu hamna huruma?Tunasikitika Kanumba ameondoka in a verry young age but my prays are with both Kanumba and also Lulu.Lulu when u get out of jail please come to America hapa utapata all the fair life not there utaangaishwa sana na maisha yako they can even take your life away.Wishing u all the best Mungu atakusaidia,stay cool peace.