Advertisements

Friday, July 8, 2016

KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI KUFUNGA MAFUNZO YA AWALI YA UASKARI MAGEREZA, KIWIRA MKOANI MBEYA

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira(pichani
Askari Wanafunzi wa Mafunzo ya Awali ya Uaskari Magereza Kozi Na. 28 ya 2016 wakiwa katika Gwaride la Maandalizi ya Sherehe za kufunga Mafunzo hayo katika Chuo cha Magereza, Kiwira Kilichopo Mkoani Mbeya. Mafunzo hayo yanatarajiwa kufungwa rasmi Julai 08, 2016.
Gadi ya Askari Wanafunzi Wanawake wakipita kwa mwendo wa pole katika Gwaride la maandalizi ya kufunga rasmi Mafunzo ya Awali ya Uaskari Magereza Kozi Na. 28 kama wanavyoonekana katika picha(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira(pichani, kesho tarehe 08 Julai, 2016 saa 3:00 asubuhi anatarajia kufunga rasmi Mafunzo ya Awali ya Uaskari Magereza Kozi Na. 28 katika Chuo cha Magereza, kilichopo Kiwira Mkoani Mbeya.

Mafunzo hayo ambayo yamechukua muda wa miezi minne yalilenga kuwaandaa Askari wa Jeshi la Magereza ngazi ya Awali ambao watatekeleza majukumu ya msingi ya kazi ambayo ni kuwapokea, kuwalinda na kuwarekebisha wahalifu tabia zao wawapo gerezani ili wamalizapo adhabu zao wawe raia wema. Jumla ya Wahitimu 1364 wanatarajia kuhitimu Mafunzo ya Awali ya Uaskari Magereza, kati yao Wanaume ni 977 na Wanawake 387 Aidha, Wahitimu hawa wote wametoka JKT. 

Sherehe hizo, zitajumuisha mambo yafuatayo:- * Mgeni Rasmi kukagua Gwaride rasmi lililoandaliwa na wahitimu hao;
* Mgeni Rasmi kutoa vyeti kwa Wanafunzi waliofanya vizuri katika Mafunzo ya Darasani na Mafunzo ya mbinu za medani na;
* Mgeni Rasmi kutoa Hotuba.

Sherehe za ufungaji wa Mafunzo hayo zinatarajia kukamilika saa 8:00 mchana. Vyombo vya Habari vinakaribishwa kwenye Sherehe hizo siku ya Jumamosi tarehe 08 Julai, 2016 kuanzia saa 3:00 asubuhi.


IMETOLEWA NA KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO
MAKAO MAKUU YA JESHI LA MAGEREZA Julai 07, 2016

No comments: