NAMSHUKURU Mungu kwa kila ambalo amekuwa akinitendea katika kila siku ya maisha yangu.
Namshukuru pia kwa kunipa uwezo wa kuandika haya ninayoandika kupitia safu hii nikiamini kuwa ni yenye manufaa makubwa katika maisha yetu ya kimapenzi.
Ndugu zangu, hivi karibuni nilikuwa nikizungumza na dada mmoja ambaye hajaolewa lakini ana mpenzi wake. Tulijadili mambo mbalimbali yanayohusu mapenzi lakini kikubwa alilalamikia suala la mpenzi wake kudai haridhiki na kile anachompatia wawapo faragha.
Namshukuru pia kwa kunipa uwezo wa kuandika haya ninayoandika kupitia safu hii nikiamini kuwa ni yenye manufaa makubwa katika maisha yetu ya kimapenzi.
Ndugu zangu, hivi karibuni nilikuwa nikizungumza na dada mmoja ambaye hajaolewa lakini ana mpenzi wake. Tulijadili mambo mbalimbali yanayohusu mapenzi lakini kikubwa alilalamikia suala la mpenzi wake kudai haridhiki na kile anachompatia wawapo faragha.
Kwa maelezo ya dada huyo ambaye kimuonekano tunaweza kusema amejaaliwa umbo na sura ya kuvutia, mpenzi wake amekuwa akimlaumu kwa kutokuwa na manjonjo wawapo kwenye uwanja wa kujidai.
Anasema: “Namshukuru Mungu kwa kunijaalia umbo lenye mvuto kwani hata nikijiangalia mwenyewe najikubali na naamini mpenzi wangu anajisikia raha kuwa na mimi lakini tatizo lipo pale tunapokutana faragha.
“Sina utaalaam kabisa wa mambo ya mapenzi ila nimekuwa nikijitahidi kutaka kujua mambo mengi ya ndani ili niweze kumridhisha mpenzi wangu.
“Lakini cha ajabu wakati nikihangaikia hilo mwenzangu ameanza kunisaliti na hata wanawake ambao wanaonekana kumzuzua nikiwaangalia nawaona hawana uzuri kunishinda mimi kabisa.”
Kwa kifupi niliongea mengi na dada huyu lakini nikabaini jambo moja tu kwamba, wanaume si watu wa kutulia na mwanamke ambaye hampi manjonjo ya kumdatisha.
Pia kuna wanawake ambao wanajiona kwa uzuri wao tu inaweza kuwa sababu tosha ya kutosalitiwa. Hawa hawajui kwamba uzuri si chochote kama mwanamke atakuwa hajui ‘majamboz.’
Ndiyo maana unaweza kushangaa mumeo anaganda kwa mwanamke mwingine ambaye hana uzuri wowote lakini kumbe mwanamke huyo anayajua mambo ile mbaya.
Mimi nadhani ni suala la kujiangalia upya katika hilo lakini leo nataka kuzungumzia jambo ambalo najua linawakera wengi ila wanashindwa tu namna ya kuwafikishia ujumbe walengwa.
Nazungumzia manjonjo waliyonayo baadhi ya wanawake kwa waume zao pale wanapokuwa kwenye uwanja wa sita kwa sita.
Kuna hili suala la miguno na mihemko ya kimahaba. Jamani hili nimelinyamazia lakini leo nimeona nilizungumzie ili kwa wale wanaoweza kubadilika, wabadilike.
Sikatai mapenzi yanahitaji utundu na ubunifu ili kila mmoja aweze kumdatisha mwenzake na hatimaye kupeana furaha ya aina yake. Hata hivyo, kuna ubunifu mwingine naweza kusema haufai hasa kutokana na mazingira tunayoishi.
Mihemko na migumo ya kimahaba kwa watu wanapokuwa faragha si jambo la kushangaza kwani hutokea kwa kila mtu, awe mwanaume au mwanamke, lakini pia wapo ambao wao ni kimya kimya tu, kelele hakuna!
Aidha, inaelezwa kuwa kuna baadhi ya wasichana hasa wale makahaba wamekuwa wakitumia njia hiyo tena kwa kujifanyisha kwa lengo la ‘kuwaibia’ wanaume wao. Hilo nalo yawezekana lipo!
Lakini sasa, ninachotaka kuzungumza hapa ni ile tabia ya baadhi ya wanawake walioolewa kutumia mbinu hiyo wakidhani eti wanawadatisha waume zao.
Mbaya zaidi wanaofanya hivyo kuna wanaoishi kwenye nyumba za kupanga kiasi kwamba wanapokuwa faragha bila kufungulia redio kwa sauti kubwa, mambo hayawezi kwenda ipasavyo.
Heri basi wale wanaoishi nyumba za kupanga na wakaweza kutumia redio ili hiyo mihemko na migumo ya kimahaba isisikike lakini kuna ambao mwenye nyumba hataki sauti kubwa, matokeo yake mchezo unakwenda hewani na kusikika laivu kwa wapangaji na watoto waliolala chumba cha pili ambao muda huo wanakuwa hawajalala.
Hili ni tatizo na kero kwa walio wengi. Hatukatai kama kweli hiyo migumo na malalamiko inatokana na raha unayoipta lakini sasa mbona imepitiliza na wengine inaonesha dhahiri mnajifanyisha mkidhani ndiyo mbinu ya kuwadatisha waume zenu?
Au unataka kuwafanya hadi na majirani na wapangaji wenzako nao wajue kuwa muda huo mnashughulika?
Huo ni ulimbukeni na kiukweli wanaume wengi wameshajua kuwa miguno na mihemko isiyo na mpangilio ikizidi wanaibiwa. Kwa maana hiyo tuangalie njia sahihi za kuwadatisha waume zetu, tusiige yale ambayo yanaweza kutufanya tukatafsiriwa tofauti na wapenzi wetu.
Usanii kweli upo kwenye mapenzi lakini ukizidi hadi mpenzi wako akakushitukia haileti picha nzuri.
Nadhani mtakuwa mmenielewa. Tukutane wiki ijayo kwa mada nyingine.
www.globalpublishers.info.
No comments:
Post a Comment