Ikulu ya White House imesema kwamba imekabili kundi la kigaidi la Al Qaida pigo kubwa kwa kumwua naibu wa mkuu wa kundi hilo, Abu Yahya al-Libi, nchini Pakistan.
Maafisa wa Marekani wamesema kuwa alilengwa katika shambulio lilolofanywa na ndege isiyo na rubani ya Marekani katika maeneo ya mashambani ya Pakistan mnamo Jumatatu.
Ikulu ya White Housae ilithibitisha kuwa hii ni mara ya pili chini ya muda wa mwaka mmoja ambapo Marekani imemwua kiongozi mkuu wa Al-Qaida, hatua ambayo inakaribia kuangamiza kundi hilo la kigaidi.
Afisa wa cheo cha juu katika serikali ya Marekani, amethibitishia BBC kuwa shambulio la ndege isiyo na rubani lililofanywa katika maeneo ya mashambani lilimlenga Abu Yahya al-Libi, ambaye alidaiwa kupanda cheo na kushikilia nafasi ya pili katika kundi hilo kufuatia kifo cha Osama Bin Laden, mwaka jana.
Obama athibisha kuawa kwa al-Libi
Serikali ya Rais Obama imethibitisha kuwa Abu Yahya al-Libi ni mmoja wa wale waliouwa katika shambulio hilo la ndege isiyo na rubani.
Wadokezi wa Serikali ya Marekani walisema kuwa kiongozi huyo wa Al-Qaida alikuwa alikuwa lengo la shambulio hilo la eneo linalodhaniwa kuwa maficho ya wapiganaji kadhaa wa Al Qaida Kaskazini mwa Wazirstan karibu na mpaka wa Afghanistan.
Marekani ilimtaja Al Libi kama anayeshikilia cheo cha pili katika kundi hilo, anayesimamia shughuli za kila siku katika eneo hilo la mashambani na maeneo mengine yaliyo na uhusiano mkubwa na kundi hilo. Afisa mmoja wa Marekani alisema kifo cha kiongozi huyo wa Al Qaida ni pigo kubwa kwa kitovu cha Al Qaida.
Ingawa Marekani imeshangilia kuuawa kwa viongozi hao wa Al Qaida na wapiganaji wa Taliban kila mara wanapotumia ndege hiyo isiyo na rubani; uhusiano wa Marekani na Pakistan umeendelea kuzorota kwa sababu ya mashambulizi hayo.
Katika mashambulizi mengine raia wamewahi kufariki kimakosa katika Pakistan na taifa jirani la Afghanistan. Serikali ya Pakistan kwa upande wake imelaumu Marekani mara kadhaa kwa kuingilia anga yake na kudharau utawala kwa kukosa kushirikiana nayo katika mashambulizi hayo.
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake