Tuesday, June 5, 2012

UN YAZUNGUMZIA UMUHIMU WA KUTUNZA MAZINGIRA KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI.

  Mratibu  wa Mpango wa Kupunguza Uzalishaji wa Hewa ya Ukaa kutokana na Ukataji miti ovyo na Uharibifu wa Misitu kwa nchi zinazoendelea (MKUHUMI) unaotekelezwa na Umoja wa Mataifa UN-REDD Bw. Ralf Ernst akisoma hotuba wakati wa ufunguzi wa Warsha ya siku moja kwa waandishi wa habari yenye lengo la  kujenga ufahamu miongoni mwao katika kuelekea kufanyika mkutano wa Maendeleo endelevu Rio+20 utakaofanyika kuanzia Juni 20-22 nchini  Brazil kwa niaba  ya Mwenyekiti wa Kikundi cha Mazingira ambaye pia ndio Naibu Mkurugenzi Mkazi wa UNDP Bi.Louise  Chamberlain. Kulia ni Gertrude Lyatuu. Kauli mbiu ya mwaka huu ni "THE FUTURE WE WANT".
 Mtaalamu wa Mazingira na Nishati wa UNDP Dkt. Amani Ngusaro akizungumza kuhusu umuhimu wa mkutano wa Rio+20 na maana yake katika kuipeleka dunia pale inapotaka kwenda. Katikati  ni Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Richard Muyungi na kushoto ni Aifsa Mkuu wa Utafiti wa Masuala ya Mazingira katika Ofisi hiyo Dkt. Constantine Shayo.
 Afisa Habari kutoka kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa Stella Vuzo akimkaribisha Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Richard Muyungi (hayupo pichani).
  Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Richard Muyungi akifafanua kuwa Tanzania kama mwanachama wa mkataba wa umoja wa mataifa wa mabadiliko ya tabianchi amesema Tanzania imeandaa  Rasimu ya Ripoti ya Rio+20 itakayojadiliwa na mkutano huo.
Bw. Muyungi alitumia fursa hiyo kuwakilisha mada kuhusiana na maendeleo endelevu ya Tanzania katika miaka 20 tangu mwaka wa kwanza kufanyika mkutano wa kwanza wa RIO iliyohusu "wapi tulipokuwa na wapi tulipo sasa".
Bw. Muyungi ameongeza kusema kuwa Mkutano huu utaainisha hatua zitakazoangalia utekelezaji na kuhuisha nguzo zote tatu za maendeleo endelevu (mazingira Uchumi na Jamii) kwa kufuata  kanuni za usawa huku tukitambua  tofauti katika uwajibikaji na uwezo.
Upatikanaji wa njia mpya, za  ziada, thabiti, zinazotabirika za kupata fedha kwa ajili ya kutekeleza shughuli za usimamizi wa mazingira na maendeleo endelevu kwa nchi zinazoendelea.
 Washiriki kutoka vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini wakiwa katika warsha inayohusiana na mkutano wa Rio+20 iliyoandaliwa na Umoja wa Mataifa katika kusheherekea maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani.

 Bi.Gertrude Lyatuu (kulia) kutoka Umoja wa Mataifa akizungumzia mfumo wa uwezeshaji utakaopelekea uzalisha, usambazaji na matumizi ya bidhaa na huduma ikiwa ni matokeo ya kuboresha maisha ya mwanadamu kwa muda mrefu kwa kutunza mazingira bila kukiangamiza kizazi kijacho.
 Mmoja wa Washiriki akichangia maoni yake kuhusiana na nini kifanyike ili waandishi wa habari waweze kuwa na ufahamu na elimu ya mazingira na kuizungumzia kwa jamii.
Mratibu wa Mpango wa Kupunguza Uzalishaji wa Hewa ya Ukaa kutokana na Ukataji miti ovyo na Uharibifu wa Misitu kwa nchi zinazoendelea (MKUHUMI) unaotekelezwa na Umoja wa Mataifa UN-REDD Bw. Ralf Ernst akielezea  Utekelezaji wa MKUHUMI ambao umejikita katika kupunguza hewa ukaa kwa kutekeleza shughuli kama vile Kuzuia ukataji miti ovyo (Deforestation), Kuzuia uharibifu wa misitu (Forest Degradation), Uhifadhi wa Misitu (Forest Conservation), Usimamizi endelevu wa misitu (Sustainable Forest Management) na Kuongeza uwezo wa misitu kuhifadhi kaboni (Enhancement of Carbon Stock).
 Juu na chini ni Baadhi ya Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali nchini walioshiriki warsha iliyoandaliwa na shirika la Umoja wa Mtaifa kuhusiana na Umuhimu wa kufahamu na kutunza mazingira ikiwa ni katika Siku ya kuadhimisha Mazingira Duniani ambapo kitaifa imefanyika mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro.
 Picha kwa hisani ya MO Blog

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake