DODOMA, TANZANIA
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetoa pole kwa wale wote ambao wamepatwa na msiba katika ajali ya meli iliyotokea jana, Zanzibar.
Pamoja
na pole, CCM imeitaka serikali kuipitia upya taarifa ya Tume
iliyoundwa kuchunguza ajali ya kwanza ya meli ya Mv. Spice Islander na
kuitaka serikali kuchukua hatua za haraka pale itakapobainika kuwepo kwa uzembe kwa watendaji wowote bila kujali nyadhifa zao.
Kauli
hiyo ilitolewa jana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM, Nape
Nnauye, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa leo
kuhusu ajali hiyo.
Nape
alisema kuna umuhimu mkubwa wa kuipitia upya kwa taarifa hiyo kwani
inawezekana kuna baadhi ya mambo hayakufuatiliwa kwa kina na au kuna
uzembe unafanyika.
Alisema
endapo kutabainika kuwepo kwa uzembe basi wale wote wanaohusika na
uzembe huo wawajibike wenyewe kwani haiwezekani watumie fedha za
wananchi lakini hakuna linalofanyika.
“Ni
Muhimu tufike wakati wewe kama kiongozi unapoona jambo limekushinda au
limetokea kutokana na uzembe na wewe kiongozi upo tujenge tabia ya
kujudhuru hii itasaidia kuleta heshima zaidi’’ alisema Nape.
Alisema
hali hiyo inatokana na ukweli kuwa mara kwa mara tukio la kuzama kwa
meli au ajali mambo mbalimbali hujitokeza ikiwemo uzito wa mizigo au
idadi kubwa kuliko uwezo wa meli au uchakavu.
Nape
alisema vyombo vinavyohusika ni lazima kuwa makini na watendaji wake
kama wameshindwa kufanya kazi ni bora wawajibike wenyewe au wawajibishwe
na mamlaka za juu.
“Sasa
meli inaondokaje bandarini ikiwa imebeba abiria zaidi au mizigo zaidi
ya uwezo wake wakati kuna watu wanaohusika na kazi hiyo, hii inatia
shaka kidogo na huko ni kuwaibia wananchi kwa kutowajibika ’’
Kwa
mujibu wa Katibu huyo alisema hivi sasa inaonekana kuwa usafiri wa
ndege umekuwa ni wa uhakika zaidi lakini hilo linatokana na ukweli kuwa
watendaji wake wamekuwa makini kila wakati.
Aidha
Nape alisema kutokana na msiba huo ulitokea CCM imehairisha Mkutano
wake wa hadhara ambao walipanga kufanyika Kigoma jana .
Alisema sasa mkutano huo utafanyika siku ya Jumapili baada ya kumalizika kwa siku za maombolezo zilizowekwa na serikali.
“Tunatoa
pole kwa wale wote waliofikwa na msiba na kwa wale ambao bado wanaugua
kutokana na jail hiyo tunamuomba Mungu awaeze kuwasaidia waweze kupona
haraka.
No comments:
Post a Comment