Thursday, August 9, 2012

AJALI YA BASI LA SABENA YAUA 17, YAJERUHI 78 MKOANI TABORA


Basi la Sabena baada ya kupata ajali.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora, ACP Antony Rutta akitoa maelezo ya ajali kwenye eneo la tukio kwa waandishi wa habari.
WATU 17 wamekufa na wengine 78 kujeruhiwa wilayani Sikonge katika Mkoa wa Tabora baada ya basi la Sabena aina ya Scania lenye namba za usajili  T570 AAM kupata ajali na kupinduka. 
Basi hilo lilikuwa likitoka Tabora kwenda Mbeya.
Ajali hiyo ilitokea katika eneo la Kitunda wilayani Sikonge umbali wa kilometa 200 kusini mwa mji wa Tabora.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, Anthony Ruta, alisema basi hilo lilikuwa limejaa kupita kiasi kwani inaonekana lilikuwa na abiria zaidi ya 100.

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake