Rais Jakaya Kikwete, ni miongoni mwa wakuu wa nchi na Serikali watakaoshiriki katika mkutano maalum wa nchi wanachama wa Taasisi ya Kimataifa ya Nchi za Maziwa Makuu (ICGLR) ulioanza mjini Kampala, Uganda, jana.
Mkutano huo wa siku mbili, utajadili hali tete ya usalama Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ambako mapigano kati ya Jeshi la DRC na kikundi cha waasi cha M23 yamesababisha zahama ya vifo na maelfu ya wakimbizi kutoka Jimbo la Kivu Kaskazini.
Inakadiriwa kuwa kiasi cha wakimbizi 30,000 wamevuka mipaka na kuingia katika Burundi na Rwanda kukimbia mapigano hayo yaliyoanza upya Aprili, mwaka huu.
Rais Kikwete na ujumbe wake, uliondoka nchini jana kwenda Uganda kwa ajili ya mkutano huo wa siku mbili na ambao umetanguliwa na mikutano ya Waratibu wa Kitaifa wa nchi wanachama wa ICGLR na ule wa mawaziri wa ulinzi na mambo ya nchi hizo.
Mkutano huo unaofanyika chini ya uenyekiti wa Mwenyekiti wa sasa wa ICGLR, Rais Yoweri Museveni wa Uganda ni matokeo ya uamuzi wa mkutano mwingine maalum wa ICGLR uliofanyika wakati wa Mkutano wa 19 wa kawaida wa Umoja wa Afrika (AU) Julai 15, mwaka huu, mjini Addis Ababa, Ethiopia.
Ilikubaliwa katika mkutano huo maalum kuitisha mkutano mwingine maalum kujadili hali hiyo.
Aidha, mkutano huo wa Addis Ababa ulielezea masikitiko yake kuhusu hali tete ya usalama Mashariki mwa DRC na kulaani vikali kuibuka na vitendo vya kikundi cha M23. Mkutano huo ulisisitiza kuwa jumuiya ya kimataifa ihakikishe haitoi msaada wa aina yoyote kwa kikundi hicho ama vikundi vingine hasi vinavyoyumbisha Mashariki mwa DRC.
Mkutano huo wa Addis Ababa pia uliunga mkono jitihada zinazoendelezwa na Serikali ya DRC kupambana na M23 na pia uliunga mkono jitihada za pamoja za DRC na Rwanda kujaribu kurekebisha hali ya usalama katika eneo la Mashariki mwa Congo.
Kikundi cha M23 kinaundwa na wapiganaji ambao walijitenga kutoka Jeshi la DRC mapema mwaka huu. Kikundi hicho kinapata jina lake kutoka tarehe ya Machi 23, mwaka 2009, wakati makubaliano yalipofikiwa kati ya Serikali ya DRC na kikundi cha waasi cha zamani cha Congres National pour la Defense du Paople (CNDP) ambacho baadaye kilikiuka makubaliano hayo kwa kukataa kujiunga katika Jeshi la Ulinzi la Congo (Fardc).

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake