Kamati Kuu hiyo imewavua uanachama madiwani wawili wa
chama hicho mkoani Mwanza kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya
ufisadi.
Madiwani waliovuliwa uanachama ni Adams Chagulani wa Kata ya Igoma na
Henry Mattaka wa Kata ya Kitangiri, wakidaiwa kukiuka katiba, kanuni na
maadili ya chama.
Mbowe alisema, baada ya Kamati Kuu kupokea taarifa ya kamati
iliyoundwa kuchunguza chanzo cha mgogoro mkoani Mwanza, wamejiridhisha
kuwa wanachama hao wanastahili kuondolewa katika chama.
“Wahusika walishapewa onyo kabla ya hatua za jana na walikuwa chini ya
uangalizi kabla ya hatua kuchukuliwa na tuliwapa nafasi ya kujieleza,”
alisema Mbowe.
Alifafanua kuwa kamati ya uongozi ya mkoa wa Mwanza nayo imevunjwa
kutokana na kushindwa kutimiza wajibu wake ipasavyo na kwamba itaundwa
nyingine kadiri ya mahitaji.
Aliongeza kuwa kutimuliwa kwa wanachama hao iwe ni onyo kwa wanachama
na viongozi wengine wa CHADEMA kuwa hawataweza kuvumiliwa wakikiuka
maadili.
CHANZO:TANZANIA DAIMA
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake