Wednesday, September 12, 2012

MARTINA KADINDA AKUTANA NA MH. BALOZI TUVAKO MANONGI NEW YORK CITY

 Mbunifu wa mavazi wa Kitanzania aliyezoeleka kwa jina la single button amekutana na balozi wa Tanzania New York MH. Balozi Tuvako Manongi ofisini kwake jijini New York jana jioni... Martin Kadinda ambaye bado yupo jijini Marekani akiudhuria New York Fashion week jana alipata nafasi ya kuzungumza na, MH balozi Tuvako Manongi ambaye alimpongeza kwa jitihada zake za kutangaza Tanzania kupitia sanaa ya ubunifu wa Mitindo, pamoja na kujifunza mengi kupitia maonesho makubwa ya mavazi ya New York fashion week,  MH Balozi Manongi aliongeza kuwa watanzania wanasimama kifua mbele wakijisifu kutokana na kazi nzuri anazozifanya Kadinda ambazo zimempelekea kualikwa Marekani katika maonyesho ya music on the catwalk, hiyo ni sifa kubwa kwake na kwa taifa lake.. aliongeza kuwa inabidi aongeze juhudi na kutengeneza njia kwa wabunifu zaidi na wasanii wengine kuweza kupeperusha bendera yetu nchi nyinginezo kubwa duniani... Martin kadinda alipata nafasi ya kutia saini kitabu cha wageni pamoja na kupiga picha na balozi na maafisa mbali mbali wa ubalozi jijini New York.  Martin Kadinda aliondoka nchini Agosti 30 kuelekea Marekani ambapo alishiriki maonyesho ya Music on the catwalk Africa New York Fashion week, baada ya hapo amekuwa akihudhuria maonyesho ya New York fashion week akiwa na mwanamitindo Flaviana Matata, Rosemary Kokuhilwa na Millen Magese ambao wao wanaishi New York.
 Martin Kadinda akipata ukodak na Mh. Balozi Tuvako Manongi Katikati na maofisa wengine wa ubalozi hapa New York City.
Designer Kadinda a.k.a single button akipata ukodak na maofisa wa ubalozi hapa New York City alivyo pata fulsa ya kutembelea na kuongea  nao mawili matatu na maofisa hao.

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake