Ndani ya kipindi cha siku saba tu tumeshuhudia unyama mwingine mbaya sana wa matumizi mabaya ya nguvu za dola unaofanywa na Jeshi la Polisi ambao umegharimu tena maisha ya Mtanzania mwingine. Tukio la juzi Jumapili linatukumbusha matukio mengine mawili ya mauaji ya raia katika mazingira yanayofanana ya polisi kuzuia mikutano au maandamano ya chama cha siasa.
Ni kama polisi sasa wameamua kutumia nguvu zisiyolingana kabisa na upinzani wanaokabiliana nao. Jumatano iliyopita katika safu hii tulikuwa na tahariri iliyobeba kichwa kisemacho ‘Ni lazima Jeshi la Polisi kuvunja
maandamano kwa risasi za moto?’
Tahariri hiyo ilikuwa ikizungumzia tukio la polisi kuua raia mmoja mjini Morogoro baada ya kutumia mabomu ya machozi na risasi za moto kuwatawanya wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa Chadema waliotaka kuandamana katika Manispaa ya Morogoro Jumatatu iliyopita. Polisi katika matumizi ya nguvu, walisababisha kifo cha Ally Nzona, kijana ambaye anadaiwa kuuawa akiwa kwenye meza ya kuuza magazeti eneo la Msamvu, Morogoro.
Wakati wananchi wakiendelea kutafakari tukio la Morogoro, juzi polisi tena wameua Mwandishi wa Habari wa Kituo cha Televisheni cha Channel 10, Daudi Mwangosi, katika kijiji cha Nyololo wilayani Mufindi, Iringa. Mazingira ya kifo hiki yamejaa utata mkubwa mno, kwani taarifa zinadai kuwa mwandishi huyo alikuwa kazini, amebeba vifaa vya kazi, kamera na polisi walimuona dhahiri shahiri.
Itakumbukwa Janauri 5, mwaka jana polisi pia waliua watu watatu kwa kile walichodai kupambana na waandamanaji wa Chadema katika jiji la Arusha. Wote waliuawa kwa risasi za moto.
Kwa bahati mbaya sana, tunasisitiza kwa bahati mbaya, matukio haya hayajachukuliwa kwa uzito unaostahili na vyombo vya mamlaka serikalini kwa sababu bado mauaji haya yanatazamwa kwa sura ya harakati za kisiasa zaidi licha ya ukweli kuwa wapo wanaokutwa na maafa haya wakipita njia tu.
Katika tahariri yetu ya wiki iliyopita tuliuliza juu ya weledi katika mfumo wa utendaji kazi wa polisi wetu. Tulisema na tunarejea hapa kwamba tunaamini polisi wetu wamefuzu vizuri, wanajua njia gani zifaazo za kukabiliana na upinzani wa wananchi ambao ama wamekataa kutii amri ya kuwataka watawanyike au hata pale wanapokamata wahalifu, wanajua ni nguvu gani itumike kukabiliana na upinzani wanaoukabili.
Tulijiuliza na leo tunajuliza tena kama polisi wetu wanatafakari sawa sawa hatua za kuchukua kukabiliana na matukio kama haya, tunaendelea kuuliza je, ni halali kabisa kwa polisi kuua tu raia kama ambavyo wimbi hili linavyoendelea kushika kasi kana kwamba wako juu ya sheria na hawawajibiki kwa vitendo vyao?
Tunauliza maswali haya kwa sababu wakati raia waliouawa Arusha na Morogoro kulikuwa na vizingizio vya kuwahusisha katika maandamano, tukio la Mwangosi linaonyesha dhahiri nia ovu ya kufanya unyama kwa sababu walimuua wakati akimtetea mwandishi mwenzake wa gazeti hili, Godfrey Mushi, ambaye alikuwa amekamatwa na polisi katika purukusani na wafuasi wa Chadema waliokuwa wamekaa nje ya ofisi za tawi la Chadema la Nyololo.
Polisi wa Iringa wanawafahamu waandishi wote hawa, yaani Mushi ambaye akikamatwa na kuachiwa baadaye, lakini hata Mwangosi wanamjua vilivyo, alikuwa mkoani Iringa, amefanya kazi na polisi kwa miaka mingi.
Kwa maana hiyo, kitendo cha kuwamiminia mabomu ya machozi waandishi waliokuwa kazini, tena wakiwa na vifaa vya kazi ni kielelezo kingine cha kuthibitisha kuwa polisi hawa hawajali, hawaheshimu taaluma nyingine zenye wajibu unaokubalika katika jamii, kama waandishi wa habari.
Kwa kila tukio la mauaji, polisi wamekuwa wakiibuka na lugha ya kujikosa, Arusha walijikosha, Morogoro ndiyo kabisa wamejikosha kwa kudai kuwa haijulikani Nzona alikufa kwa kitu gani, lakini wanadai siyo risasi, Iringa nako madai ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Michael Kamuhanda, hayatofautiani na ya Morogoro, kujikosha.
Tunafahamu kabisa kwamba vyombo vya habari viko kwa ajili ya kuhabarisha umma, waandishi wanafanya kazi katika mazingira magumu na hatarishi sana, lakini ni vigumu kuvumilia kitendo cha polisi kuua mwandishi wanayemfahamu, mwenye utambulisho wa wazi kabisa lakini pia katika kile kinachoonekana ni nia ovu ya kufunika taarifa alizokuwa anarekodi zisiwafike wananchi wengi zaidi.
Tunaungana na wanadau wote wa habari kulaani mauaji haya, na kwa kweli tunataka uchunguzi huru ufanyike juu ya tukio hilo ovu dhidi ya tasnia ya habari kwa ujumla wake.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment