Mkuu
wa Itifaki wa Miss Tanzania Albert Makoye akifungua mashindano ya
Redd's Miss Kinondoni Talent, pembeni yake ni Ssebo ambaye ni mmoja kati
ya mwanabodi wa Redd's Miss Kinondoni 2012 na alikuwa ni mshereheshaji
katika shindano hilo lililofanyika katika hoteli ya JB Belmonte, iliyopo
jengo la Benjamin Mkapa, Dar es Salaam. Mashindano hayo yalidhaminiwa
na Perfect Lady Classic Saloon iliyopo Kinondoni jijini Dar na wametoa
zawadi kwa washindi watatu waliopatikana kwa kupewa huduma kwa kipindi
cha mwaka mzima ndani ya Saloon yao. Shindano rasmi la kumsaka Redd's
Miss Kinondoni linatarajiwa kufanyika Ijumaa tarehe Septemba 14, 2012
katika Ukumbi wa Cassa Complex uliopo Mikocheni, Dar
Mshiriki namba 6, Irene akionyesha manjonjo yake katika kucheza.
Brigitter Alfred mshiriki namba 9 alionyesha umahili wake katika nyimbo za kihindi.
Mshiriki namba 4, Diana Hussein akionyesha jinsi ya kubuni vazi.
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake