ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, October 2, 2012

MAZISHI YA BABA MZAZI WA EDWARD WAIGAMA

Picha ya marehemu mzee Steven Waigama Baba ya Edward Waigama aneishi Maryland Nchini Marekani Baba yake alifariki Sept 3, 2012 Nyamongo, Tarime mkoani Mara na kuzikwa Sept 7, 2012 hapo hapo Nyamongo.

Edward kwa niaba yake, mkewe na familia ya Waigama watatoa shukrani kwa ndugu, jamaa na marafiki walioshiriki kwa hali na mali katika kufanikisha msiba huu mkubwa wa kumpoteza baba mzazi.

Shukrani za pekee kwa marafiki wote ninaoishi nao hapa Marekani kwa kuweza kuacha shughuli zao na kufika nyumbani kunipa pole hasa kwa taarifa ya muda mfupi iliyowafikia  na mimi nilikua nasafiri kesho yake kuwahi mazishi ya mpendwa baba yangu nashukuru sana kwa hilo na najivunia kuwa na marafiki wenye upendo wa kweli, Mungu awabariki sana na awaongezee maradufu.
 Siku Edward Waigama alipowasili Nyamongo tayari kumsindikiza baba yake mzazi kwenye safari yake ya mwisho kwenye nyumba yake ya milele
 Ndugu jamaa na marafiki waliofika kwenye msiba wa Mzee Steven Waigama
 Jeneza lililobeba mwili wa Mzee Waigama likipelekwa kwenye nyumba yake ya milele
 Picha juu na chini ni Ndugu, jamaa na marafiki waliofika kwenye mazishi ya mzee Waigama

Ndugu wa karibu na familia akielezea utaratibu wa kuaga mwili
 Edward akiaga mwili wa Mzee Waigama.
 Nyumba ya milele ya Mzee Waigama
 Mzee waigama akiingizwa kwenye nyumba yake ya milele
Mashada ya maua yaliyowekwa juu ya kaburi
Edward akipata picha kwenye kaburi la Mzee waigama

No comments: