NI takriban Kilometa 60 kutoka Ikwiriri hadi kufika iliko Shule ya Sekondari Ruaruke iliyopo Kata ya Ruaruke Wilaya ya Rufiji, mkoani Pwani.
Usafiri wa kuaminika kuelekea huko ni pikipiki ambazo pamoja na kuwa nauli yake ni ghali, ndio unaoweza kukufikisha huko.
Ili ufike Ruaruke utalazimika kupita katika vijiji vya Mchukwi A, Mchukwi B na Nyamatanga. Shule hiyo ipo kati ya vijiji vya Ruaruke A na Ruaruke B.
Safari yangu ya kuelekea katika shule ya sekondari ni taarifa zilizochapishwa na gazeti hili hivi karibuni, kuhusu hali ya kusikitisha inayowakabili walimu wa shule hiyo iliyojengwa kwa nguvu za wananchi kuanzia mwaka 2001 na kukamilika 2004.
Shule ya Sekondari Ruaruke imekuwa ikipokea wanafunzi wa vijiji mbalimbali vya Kata ya Ruaruke na kata nyingine za jirani.
Wakazi wengi wa Kata ya Ruaruke ni wakulima na wafanyabiashara ndogondogo. Kilimo kikuu eneo hilo ni pamoja na muhogo, mpunga, mahindi na mazao jamii ya kunde.
Hata hivyo, wakazi wengi wanaisha maisha duni, kiasi kwamba ni familia chache zinazomudu kula milo mitatu kwa siku.
Hata hivyo, wakazi wengi wanaisha maisha duni, kiasi kwamba ni familia chache zinazomudu kula milo mitatu kwa siku.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Ruaruke A, Suleiman Mfaume anasema kwa sababu wanafunzi wengi wanaishi mitaani wakijitegemea, ni vigumu kubaini na hata kudhibiti mienendo yao isiyofaa.
“Uvutaji bangi na ngono ni jambo lisiloepukika kwa baadhi ya vijana, kwani hakuna wa kuwalinda kutokana na wao kuishi wakiwa huru bila ulinzi wa wazazi wao, “anaeleza.
“Uvutaji bangi na ngono ni jambo lisiloepukika kwa baadhi ya vijana, kwani hakuna wa kuwalinda kutokana na wao kuishi wakiwa huru bila ulinzi wa wazazi wao, “anaeleza.
Mandhari ya shule
Unapofika shuleni hapo na kutupa jicho katika baadhi ya kuta za majengo, ukionacho kinatosha kukupa picha halisi ya aina ya wanafunzi wanaosoma hapo.
Unapofika shuleni hapo na kutupa jicho katika baadhi ya kuta za majengo, ukionacho kinatosha kukupa picha halisi ya aina ya wanafunzi wanaosoma hapo.
Kwa mfano, baadhi ya kuta sasa zimepambwa na kila aina ya michoro ya kudhalilisha, lugha za kejeli, maudhi na hata matusi kwa walimu hasa Mkuu wa Shule ambaye katika maandishi mengi ukutani amekuwa akitajwa kwa jina la Ngozi.
Baadhi ya matusi hayaandikiki gazetini, lakini kwa kuta za Shule ya Sekondari Ruaruke, hilo limewezekana. Walioandika bila shaka walifanya hivyo kuonyesha hisia zao kwa mtu wanayemtaja kuwa ndiyo adui yao.
Miongoni mwa maandishi hayo, kulikuwa na haya yaliyosema: ‘baada ya mwalimu mkuu bado mwalimu Moyanga’
Kwa kuwa ziara yangu niliifanya siku chache baada ya vurugu kutokea shuleni hapo, macho yangu hayakusita kuona mabaki ya viti vilivyoharibiwa madarasani, nyumba ya mwalimu mkuu iliyovunjwa na majengo yaliyochomwa moto.
Kwa hakika shule ilikuwa imetelekezwa, mazingira yake hayavutii kuyatazama. Kukosekana kwa watu wanaoishi hapo, kumetoa mwanya kwa majani kuota kwa kasi katika eneo la shule kiasi cha kusababisha pori la aina yake.
Kitaaluma hali si nzuri katika shule hiyo. Kwa mfano, katika matokeo ya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2011 wahitimu 74 kati ya 91 walipata daraja sifuri, 14 walipata daraja la nne.
Walimu waikimbia shule
Taarifa za awali zilizoandikwa na gazeti hili zinasema walimu waliamua kuikimbia shule hiyo baada ya kukithiri kwa vitenda vya unyanyasaji kimapenzi kwa walimu wa kike na vitisho.
Taarifa za awali zilizoandikwa na gazeti hili zinasema walimu waliamua kuikimbia shule hiyo baada ya kukithiri kwa vitenda vya unyanyasaji kimapenzi kwa walimu wa kike na vitisho.
Aidha, taarifa zilieleza kwamba walimu hao walilazimika kuikimbia shule hiyo baada ya baadhi ya walimu wa kike kutongozwa na wanafunzi,kubakwa, kupigwa mabusu kwa nguvu hadharani, kutishiwa kuchomwa visu na kuchorwa vikatuni vya kudhalilisha.
Baadhi ya walimu, watendaji wa kata, Mkuu wa Wilaya ya Rufiji na Mbunge wa Kibiti walithibitisha ukweli wa suala hilo walilosema wanalifahamu na kwamba wapo kwenye mchakato wa kulipatia ufumbuzi.
Wanafunzi wazungumza
Mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo anayesoma kidato cha tatu, (jina tunalihifadhi) anasema kwanza ieleweke kuwa vurugu hazikusababishwa na wanafunzi wachache wanaotuhumiwa.
Mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo anayesoma kidato cha tatu, (jina tunalihifadhi) anasema kwanza ieleweke kuwa vurugu hazikusababishwa na wanafunzi wachache wanaotuhumiwa.
Hatua ya kufanya fujo anasema ilitokana na uamuzi wa wanafunzi wote baada ya kuchoshwa na vitendo vya unyanyasaji walivyokuwa wakifanyiwa na walimu. Anasema hata pale baadhi yao walipowashtaki walimu hao katika bodi ya shule, hakuna hatua zilizochukuliwa. “… shule nzima hivyo ni vyema shule nzima ikashitakiwa kwa kuwa wanafunzi waliamua wote kufanya vurugu. Kushitakiwa watu wachache ni kuwaonea,’’anasema na kuongeza:
“Sababu kubwa ya kufanya vurugu ni tabia ya walimu kutupiga kwa kutumia ngumi, mateke na kutoingia madarasani na walimu kutoa adhabu kali wakati madarasani hawaingii, bali wanatoa notisi tu, Walimu wamekuwa wakali sana na wamekuwa wakitoa adhabu kali wakati madarasani hawaingii, hivyo sisi tukaona njia mwafaka ni kufanya vurugu ili kukomesha unyanyasaji huo.’’
Dai lao lingine wanafunzi hao wanasema ni shule kukosa walimu wa sayansi kwa muda mrefu.
Hata hivyo, uchunguzi wa Mwananchi umebaini tabia mbaya za baadhi ya wanafunzi, zina baraka za wazazi wao wanaoshindwa kuwakemea.
Hata hivyo, uchunguzi wa Mwananchi umebaini tabia mbaya za baadhi ya wanafunzi, zina baraka za wazazi wao wanaoshindwa kuwakemea.
Kibaya zaidi wazazi hao huja juu pale watoto wao wanapoadhibiwa na walimu.
Mwananchi
No comments:
Post a Comment