Mkurugenzi wa Biashara wa CFAO Motors Wayne Mcintosh akizindua rasmi gari ya Nissan Patrol aina ya Y62 leo katika makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam.
Katika uzinduzi huo wa gari hiyo mpya ambayo ni Four Wheel Drive yenye uwezo wa kubeba watu 8 na yenye nguvu ya 5.6L V8 injini yenye spidi ya 240 ni ya pekee duniani kuzinduliwa na Tanzania inakuwa ya kwanza katika nchi za Afrika Mashariki na kati kuingia baada ya Congo DRC, Angola na Ghana.
Bw. Mcintosh amesisitiza kwamba gari hii inaviburudisho pamoja na Tv katika hali ya kumsaidia dereva kwenye safari ndefu.
Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya CFAO Motors na wageni waalikwa wakimsikiliza Bw. Wayne Mcintosh (hayupo pichani) kwenye uzinduzi huo.
Meneja Masoko wa Kampuni ya CFAO Motors Tharaia Ahmed (wa pili kulia) na baadhi ya wageni waalikwa.
Mkurugenzi wa Biashara wa CFAO Motors Wayne Mcintosh akiendesha bahati nasibu ya kwenda kushuhudia fainali na Michuano ya kombe la Mataifa barani Afrika inayofanyika nchini Afrika kusini kwa wageni waliohudhuria uzinduzi huo.
Mkurugenzi wa Biashara wa CFAO Motors Wayne Mcintosh akitangaza washindi wawili watakaoenda nchini Afrika Kusini kushuhudia fainali za mashindano ya AFCON.
Mkurugenzi wa Biashara wa CFAO Motors Wayne Mcintosh akimpongeza mshindi wa shindano la bahati nasibu Group Manager wa DELFINA Bw. Sajjad Dharamsi atakayeenda nchini Afrika Kusini kushuhudia fainali za mashindano ya michuano ya AFCON 2013. Kushoto ni Meneja Masoko wa CFAO Motors Tharaia Ahmed.
Kwa picha zaidi bofya read more
Bw. Wayne Mcintosh akimpongeza mshindi wa pili wa Kampuni ya Wambi Lube Oil Distributor Bw. Omari Omari.
Peer Educator wa CFAO Motors Maria Petro (kulia) akimpongeza Bw. Omari Omari kwa kushinda droo ya kwenda kutizama fainali za AFCON 2013 nchini Afrika Kusini iliyoendeshwa na kampuni hiyo wakati wa hafla ya uzinduzi wa gari mpya aina ya Nissan Patrol Y62. Katikati ni Meneja Masoko wa CFAO Motors Tharaia Ahmed.
Afisa Mauzo wa CFAO Motors Magdalena Mpeku akitoa maelezo ya gari mpya aina ya Nissan Patrol Y62 kwa baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria uzinduzi huo.
Meneja Masoko wa CFAO Motors Tharaia Ahmed akizungumza na mmoja wa wateja wakati wa uzinduzi wa gari aina ya Nissan Patrol Y62 makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar.
Wageni waalikwa wakila na kunywa wakati wa hafla hiyo.
Warembo waliokuwa wakikaribisha wageni wakipozi kwenye gari hiyo mpya aina ya Nissan Patrol Y62.
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake