Monday, February 4, 2013

Hapa na pale Waume wa Uswazi na vifo vya Mapema


Hili ni jambo ambalo nimelishuhudia zaidi ya maeneo matano lakini nimeambiwa pia kuhusu maeneo mengine ya Uswazi nako ni hivyo hivyo.
Ni kwamba asilimia 80 ya maeneo mengi ya Uswazi wanawake wengi ni wajane,yaani wengi wa akina mama wanaoishi maeneo hayo wamefiwa na waume zao.
Hii ina maana kuwa ukikutana na wanawake 10 kati ya 8 waliowahi kuolewa kwenye maeneo mengi ya Uswazi ni wajane.
Lakini wanaume wanaoonekana kufariki ni wale waliofanikiwa kupata mafanikio kidogo.Karibu wote waliofariki walikua wana nyumba na biashara zingine kidogo kama maduka yale ya rejareja n.k.
Mfano,Mtaa ninaoishi una nyumba 25,20 kati ya hizo wanaozimiliki ni wanawake wajane,yaani wamefiwa na waume zao.
Nilikokua naishi siku za nyuma nako ni hivyo hivyo,wengi ni wamama ni wajane.
Kwanini?
Kwanini waume wa maeneo hayo hufa mapema?
Na ni kwanini wanaofariki wote hali zao za kimaisha zinafanana?Yaani wale walio na hali za chini kabisa wapo na wake zao mpaka wengine wamezeeka.
Kwanini?
Mimi sina jibu la moja kwa moja labda wewe unaweza kunisaidia!

1 comment:

  1. Kiujumla iko hivi. kila binadamu amepewa umri wa kuishi katika dunia Mungu. sasa nini inatokea mfano mwanaume mmoja amepewa kuishi dunian kwa miaka 48, ana amua kuoa akiwa na miaka 30. anamuoa mwanamke mwenye umri wa miaka 20 ambaye naye umri wake wa kuishi ni iaka 42. ni wazi kuwa mwanaume atafikia umri wake wa kuishi duniani kabla ya mwanamke. kwahiyo basi tunaweza kusema wanaume wengi wanaoa wakiwa na umri mkubwa na wanaoa wanawake wadogo kuanzia miaka 25 kushuka chini. kwa ufupi ndo hivyo nitakutumia maelezo mengine zaidi.

    ReplyDelete

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake