Mwenyekiti na Katibu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph na Asaa Rashid. Mabaraza ya Katiba kufanyika Juni -Agosti. “Hatua hiyo ni muhimu kwani Tume kupitia mikutano ya Mabaraza ya Katiba inahitaji ushirikiano mkubwa kutoka kwa wananchi. Mikutano hiyo itakuwa ya kujadili Rasimu ya Katiba itakayowasilishwa na Tume ambapo kupitia Mabaraza hayo itawezesha kupatikana kwa maoni ya (kuiimarisha) kuiboresha rasimu hiyo,”alisema Jaji Warioba na kuongeza;
MWENYEKITI wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amesema mikutano ya Mabaraza ya Katiba itaanza rasmi Juni na kumalizika Agosti mwaka huu.Hatua hiyo inakuja baada ya Tume hiyo kumaliza kazi ya kukusanya maoni kutoka kwa makundi maalumu ambapo kazi hiyo ilifanyika kuanzia Januari 7 hadi Januari 28 mwaka huu na kuhusisha makundi mbalimbali na baadhi ya watu mashuhuri.
Taasisi nyingine zilizokutana na Tume hiyo ni pamoja na Taasisi 22 za kidini, Asasi 72 za kiraia , Taasisi za Kiserikali 71, viongozi, watu mashuhuri 72 kutoka Tanzania Bara na Visiwani pamoja na vyama vya siasa 19. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Jaji Warioba alisema baada ya kumalizika kwa hatua ya ukusanyaji maoni kutoka kwa makundi maalumu hatua inayofuata ni kuundwa kwa Mabaraza ya Katiba kwa ajili ya kupitia na kutoa maoni juu ya Rasimu ya Katiba itakayoundwa na Tume.
“Hatua hiyo ni muhimu kwani Tume kupitia mikutano ya Mabaraza ya Katiba inahitaji ushirikiano mkubwa kutoka kwa wananchi. Mikutano hiyo itakuwa ya kujadili Rasimu ya Katiba itakayowasilishwa na Tume ambapo kupitia Mabaraza hayo itawezesha kupatikana kwa maoni ya kuiborsha rasimu hiyo,”alisema Jaji Warioba na kuongeza;
“Tunatarajia kuingia katika hatua nyingine ambayo ina umuhimu mkubwa katika kuunda Katiba Mpya, hatua hiyo ni kufanyika kwa mikutano ya Mabaraza ya Katiba ambayo itafanyika nchi nzima.”
Jaji Warioba alitoa wito kwa wananchi wote kushiriki kikamilifu katika kuwapata wajumbe watakaoshiriki katika Mabaraza ya Katiba kwa mujibu wa mwongozo ambao Tume umeutangaza kupitia vyombo vya habari na kusambazwa katika wilaya zote nchini.
Alisema muundo wa Mabaraza ya Katiba utazingatia mgawanyiko wa kijiografia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pia Mabaraza hayo yatawashirikisha na kuwakutanisha wawakilishi kutoka makundi mbalimbali ya wananchi katika jamii kwa lengo la kutoa maoni juu ya Rasimu ya Katiba.
“Mabaraza ya Katiba yatakuwa katika makundi mawili yaani Mabaraza ya Katiba ya Wilaya ambayo ni ngazi ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa na kundi la pili ni Mabaraza ya Katiba ya Asasi, Taasisi na Makundi ya Watu.
Jaji Warioba alisema wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya kwa upande wa Tanzania Bara katika mikoa yote watapatikana kwa kupigiwa kura za kupendekezwa kwenye ngazi ya Kijiji au Mtaa na baadaye watachaguliwa kwenye ngazi ya Kata na kwa upande wa Zanzibar, wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya itakuwa ni Shehia na kisha watapigiwa kura kwenye ngazi ya Shehia.
Chanzo; Mwananchi
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake