Wiki iliyopita tulianza kuichambua mada hii ya makundi ya wanawake na mitazamo yao kwa wanaume, leo tunaendelea na sehemu ya pili kuanzia pale tulipokuwa tumeishia. Eti namna ambavyo ile miwani inamtoa, kwake hoi.
Hata utembeaji na mikogo yake, sauti na jinsi mtu anavyoongea, vinaweza kushawishi wanawake ndani ya kundi hili. Kimsingi, wanawake ndani ya kundi hili, huvutiwa kimapenzi kwa wanaume kutokana na muonekano wao au msemo wa kisasa ni kuwa swaga za mtu ndizo ambazo zinaweza kumpa alama ya kupendwa au kupotezewa.
TATHMINI KIMAPENZI
Wanawake wa kundi hili huwa na rangi mbili. Ya kwanza ni kwamba wanazo alama nyingi za kupenda. Anapompata yule anayemmulika, humpa mapenzi yote na kila kitu ambacho mwanaume atakuwa anakihitaji. Rangi ya pili ni kuwa kama mwanamke mwenyewe ni mapepe, basi anaweza kuhamisha upendo kutokana kwa mwanaume mmoja hadi mwingine.
Kama alimpendea urefu, warefu wapo wengi, ikiwa ni mavazi, wavaaji wamejaa kila kona, vivyo hivyo kwa sifa nyinginezo. Mwanaume anapaswa kutathmini mwanamke wake yupo vipi.
Utulivu wake unaweza kuwa kichocheo cha penzi la kudumu, umapepe ni kielelezo hatarishi katika uaminifu. Ukweli ni kwamba wale watulivu huwa na mapenzi ya kweli lakini kasoro yake ni kuwa dunia inageuka, kama alikupendea gari, kuna siku unaweza usiwe nalo, hapo atakuacha. Kama ni sura, basi unaweza kupata ajali, ile ‘baby face’ iliyomvuta haitakuwepo tena.
BAHATI MBAYA
Wanawake wa kundi hili huwa na bahati mbaya moja kubwa ambayo ni usalitiwa na wanaume. Sababu ni kuwa wanaum hao mara nyingi hutawaliwa na kiburi kwamba wao ni wazuri na wanapendwa, kwa hiyo hukosa msimamo na utulivu wa kweli. Kwa vile hupenda kulelewa, hutoka na wanawake wengine ambao wataonekana wana fedha zaidi. Kadhalika, hujiona wao ni tabaka maalum sana, kwa hiyo huwa wanataka wanyenyekewe hata kama ni kwa jambo ambalo linawahitaji kunyenyekea.
Wenye tabia ya kupenda wanaume kutokana na muonekano wapo wengi, kwa hiyo unaweza kupenda kesho yake asubuhi mwingine naye akamtaka mwanaume huyohuyo wa kwako, hivyo kuleta ushindani wa kimaslahi kati ya mwanamke mmoja na mwingine. Itaendelea wiki ijayo.
www.globalpublishers.info
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake