Thursday, February 7, 2013

MELI YA MV VICTORIA ILIVYONUSURIKA KUTEKETEA KWA MOTO JIJINI MWANZA

Maafisa wa kikosi hicho walijitosa kuhakikisha moto huo hausambai katika maeneo mengine ya Meli ya Mv Victoria ambapo walifanikiwa kuuzima huku ukiwa tayari umeteketeza magodoro yote pamoja na mito ya makochi iliyokuwa katika chumba cha kuhifadhia mizigo.
Juhudi zikiendelea kwa maafisa wa kikosi hicho kuhakikisha moto huo hausambai katika maeneo mengine ya Meli ya Mv Victoria.
Maafisa wa kikosi hicho hapa wamefanikiwa kuzama chini ghalani melini humo kunyunyiza maji zaidi kuhakikisha moto huo hausambai katika maeneo mengine ya Meli ya Mv Victoria.
Maafisa wa kikosi hicho hapa wamefanikiwa kuzama chini ghalani melini humo kunyunyiza maji zaidi kuhakikisha moto huo hausambai katika maeneo mengine ya Meli ya Mv Victoria.
Hata hivyo moto huo uliodumu kwa saa kadhaa ulifanikiwa kuzimwa ndipo juhudi za kuyatoa magodoro na mito yote ya makochi yaliyokuwemo ndani ya hifadhi ya mizigo ili kuhakiki uharibifu pamoja na kufanya tathimini kwa mali zilizo haribika.
kwa picha zaidi bofya read more
Kwa umakini zaidi kuhakiki moto huo.
Wafanyakazi wa MSC wakitumia mashine maalumu ya kushushia mizigo ya kampuni hiyo wakitoa mabaki ya vitu vilivyounguzwa na moto.
Juhudi za ushushaji mizigo iliyoungua zikiendelea.
Ndani ya masaa mawili moto huo ulikuwa umedhibitiwa na kikosi cha zima moto na uokoaji waliowasili katika eneo hilo muda mchache baada ya moto kuanza wakitumia gari lenye namba za ausajili STK 1965 Mali ya Halmashauri ya jiji la Mwanza.
---
MELI ya Mv Victoria inayomilikiwa na Kampuni ya huduma za Meli nchini (MSC) imenusurika kuteketea kwa moto uliozuka wakati mafundi wa kampuni hiyo wakichomelea eneo la shimo la kuhifadhia mizigo la mojawapo ya maeneo kwenye Meli hiyo.
Moto huo uliozuka katika meli hiyo ulizua tafrani kwa wakazi wa jiji la Mwanza na kufurika katika eneo la maegesho ya Meli za Kampuni ya MSC yaliyopo katika bandari ya Mwanza kaskazini majira ya saa 8 na dakika kadhaa na kusababisha msongamano mkubwa katika eneo hilo.
Kwa mujibu wa taarifa zilizo naswa toka kwa wafanyakazi wa Meli hiyo ambao hawakutoa ushirikiano kuzungumza na waandishi wa habari, zilizonaswa wakati wakilaumiana zimeleeza kuwa mafundi wa kampuni hiyo walikuwa wakichomelea katika moja ya vyumba vya chini vya Meli hiyo ndipo cheche za moto zilipopenya na kuangukia katika sehemu ya pili ya kuhifadhia mizigo na kuanza kuwaka.
Sehemu hiyo ya mizigo kulikuwa kumehifadhiwa shehena ya magodoro pamoja na mito ya makochi tayari kwa ajili ya kusafirishwa kwenda mjini Bukoba Mkoani Kagera leo usiku.

CHANZO: GSENGO BLOG

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake