Tuesday, February 5, 2013

MKURUGENZI WA UNESCO AZUNGUMZA NA MAWAZIRI ZANZIBAR

 Juu na chini ni Mkurugenzi Mkuu wa Unesco Irina Bokova akizungumza na Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar huko katika Hoteli ya Serena ikiwa ni muendelezo wa Ziara yake ya Siku mbili Zanzibar.
 Mkurugenzi Mkuu wa Unesco Irina Bokova kulia akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mji Mkongwe Issa Sariboko hayupo pichani akitoa maelezo kuhusu Maendeleo ya Mji wa Zanzibar.hapo Serena Hotell.
 Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk kushoto akipokeya Zawadi kutoka kwa  Mkurugenzi Mkuu wa Unesco Irina Bokova walipomaliza Mazungumzo hapo katika Hoteli ya Serena ikiwa ni muendelezo wa Ziara yake ya Siku mbili Zanzibar.
 Mkurugenzi Mkuu wa Unesco Irina Bokova wakwanza kushoto akizungumza na Waandishi wa Habari mbalimbali hapo katika Hoteli ya Serena ikiwa ni muendelezo wa Ziara yake ya Siku mbili Zanzibar
-Mkurugenzi Mkuu wa Unesco Irina Bokova katikati akiwa katika Picha ya  pamoja na Mawaziri wa Serikali ya Zanzibar na Viongozi mbalimbali baada ya kumaliza kwa Mazungumzo yao katika Hoteli ya Serena ikiwa ni muendelezo wa Ziara yake ya Siku mbili Zanzibar

Na SALMA SAID, ZANZIBAR

 SHIRIKA la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) limefurahishwa na juhudi za kudumisha na kuendeleza uhifadhi wa Mjimkongwe mjini Zanzibar. Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Irina Bokova alisema mjini hapa jana  maendeleo yote mapya yanayotokea katika mji huo yanafanyika  kwa kulinda sura ya majengo ya kale kwa manufaa ya urithi.
Irina ambaye ni mwanamke wa kwanza kuongoza shirika hilo, alisema hayo baada ya ziara ya siku moja visiwani Zanzibar ambayo ni ya kwanza tangu alipoteuliwa mwaka 2009. Alisema ingawa juhudi ya kulinda Mjimkongwe inakabiliwa na changamoto mbali mbali, uendelezaji wa mji huo unafanyika kwa vigezo vinavyozingatia maendeleo ya miji ya kale duniani, vilivyowekwa na UNESCO.
Uhifadhi wa Mjimkongwe kwa vigezo vya UNESCO, unasimamiwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Uhifadhi wa Mjimkongwe (STCDA) unalinda pamoja na mambo mengine, muundo wa mitaa na majengo ya kale yenye usanifu wa asili ya  Kiswahili, Kihindi, Kiarabu na Ulaya.
Vibeke Jensen, Mwakilishi wa UNESCO nchini Tanzania, alisema katika mahojiano kuwa pamoja na uhifadhi wa mji huo, msaada wa shirika lake kwa Zanzibar ni wa muda mrefu na unagusa maendeleo ya sekta ya elimu, utamaduni,  wanawake na watoto,  utamaduni na vyombo vya habari vya kijamii.
Alisema kupitia mpango wa Umoja wa Mataifa wa Misaada ya Maendeleo (UNDAP), mwaka huu kwa pamoja sekta jizo zitanufaika na msaada wa Dola za Marekani 120,000, kulinganisha na Dola 100.000 mwaka jana.
Mapema ujumbe wa viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ukiongozwa na Wazuri wa Habari, Said Ali Mbarouk ulikuwa na mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu huyo wa UNESCO katika Hoeli ya Serena mjini hapa.

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake