Msanii wa filamu Tanzania Jackline Wolper hatimaye amefichua siri ya urembo wake kitu kinachomfanya aendelee kuonekana kuwa mrembo na kubaki na mvuto wake wa asiri
Akizungumza na Pro-24 ,Wolper alijikuta akiweka wazi anachokifanya ili kuendelea kubaki na urembo huo huku akisisitiza kuwa mazoezi ya viungo vya mwili na kutokunywa bia ni siri kubwa ya urembo wake
Wolper hakusita kuweka wazi kuwa yeye ni mtu wa kula mbogamboga,samaki, maziwa na matunda kwa wingi huku akipata muda wa kupumzika ili kujenga mwili wake bila ya kusahau kunywa maji kwa wingi kwani hayo yanamfanya ngozi yake iendelee kuwa yenye mvuto.
Wolper alisisitiza kuwa katika maisha yake hutumia kula nyama nyeupe na kuepuka nyama nyekundu ili aendelee kubaki hivyo alivyo na kuepuka kuwa mnene na kutoka kitambi kama baadhi ya wanawake wengine wanavyokuwa
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake