Monday, February 4, 2013

NCCR-MAGEUZI YAIBOMOA CHADEMA MBEYA


Moses Mwasubira, ambaye alikuwa mwenezi wa Chadema wilaya ya Mbeya akikabidhiwa kadi ya NCCR na 
Mmoja wa kada Chadema, Emanuel Mwangoka (Cash Money), ambaye inadaiwa kuwa ndiye alikuwa mfadhili Mkuu wa mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (Chadema), akikabidhiwa kadi ya chama kipya, alisema atatumia uwezo wake wote kama alivyofanya kwa sugu kuhakikisha NCCR-Mageuzi inaibuka na kung’ara mkoani 
Mjumbe wa Halmshauri Kuu taifa ya chama hicho, Juju Danda,

Mjumbe wa Halmshauri Kuu taifa ya chama hicho, Juju Danda, katika tukio la kuwapokea wanachama wapya 21 waliojunga na chama hicho, wakitokea Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Aliyewahi kuwa Katibu wa Chadema Mkoa wa Mbeya na kujiunga na NCCR-Mageuzi , Januari 20 mwaka huu Eddo Mwamalala, alisema wanachama hao waliomfuata ni mtaji mkubwa wa kuhakikisha inakimaliza chadema mkoani hapa.

CHAMA cha NCCR-Mageuzi, kimesema taifa limepoteza muelekeo kutokana na viongozi wake wengi waliopewa dhamana ya kuongoza kushindwa kutimiza wajibu wao, hali ambayo imesababisha wananchi kuishi katika mkanganyiko mkubwa.

Hayo yalisemwa jana, Jijini hapa na Mjumbe wa Halmshauri Kuu taifa ya chama hicho, Juju Danda, katika tukio la kuwapokea wanachama wapya 21 waliojunga na chama hicho, wakitokea Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Akizungumza katika mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Double J, mbele ya waandishi wa habari, Danda alisema ili taifa liweze kupiga hatua za kimaendeleo ni lazima liwe na siasa safi na uongozi bora.
Alisema kutokana na dhana hiyo kukosekana kwa viongozi waliopewa dhamana ya kuongoza kumesababisha kuliacha taifa na wananchi wake wakiishi katika mkanganyiko mkubwa unaotokana na kupanda kwa gharama za maisha.
“Vyakula vimepanda, kadhalika nauli…. Kwa ujumla gharama za maisha imepanda sana nahii yote imesababishwa na taifa kukosa watu wa kufanya siasa safi ambazo zingetuletea viongozi bora” alifafanua Danda.

Alisema msingi pekee wa taifa kupata maendeleo ni rasilimali watu ambayo imejengwa kwa kupewa elimu, hivyo kitendo cha serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kukosa mitaala ya elimu ni inaonesha taifa lilivyokosa muelekeo.
“Rasilimali watu ni muhimu katika mchakjato wa maendeleo kuzidi hata hayo madini, lakini umeona kilichotokea juzi pale bungeni…. Mwenyekiti wetu (Jems Mbatia-NCCRA-Mageuzi) alichokieleza na kilichotokea”.



Aliongeza kuwa licha ya CCM iliyoiweka serikali madarakani kujipambanua kwa itikadi ya ujamaa na kujitegemea, lakini serikali hiyo imeshindwa kuisimamia hivyo kufanya taifa kushindwa kujitegemea na badala yake limegeuka kuwa ombaomba.
Alisema hali hiyo inajidhihirisha kwenye bajeti ya serikali, kwani zaidi ya asilimia 40 ya bajeti hiyo inategemea msaada wa wafadhili jambo linalokinzana na mfumo wa itikadi yake iliyojiwekea kama malengo wakati ikitafuta dhamana ya kupewa nafasi ya kuongoza nchi.
Kwa upande wake mwakilishi wa kundi la wanachama 21 waliohamia ndani ya NCCR-MAgeuzi, Moses Mwasubira, ambaye alikuwa mwenezi wa Chadema wilaya ya Mbeya Mjini, alisema wamefikia uamuzi huo kutokana na sababu mbalimbali.
Miongoni mwa sababu hizo ni kudai kuwa uongozi wa taifa wa Chadema kushindwa kujenga Demokrasia ya kweli ndani ya chama kwa kukumbatia ufisadi wa kutumia vibaya ruzuku ya chama na kuwaacha wa mikoani wakifanya kazi kubwa ya kuchangisha fedha.
Uongozi mbaya wa Katibu Mkuu wa chama hicho taifa,Dk.Willbroad Slaa na Mwenyekiti wake Freeman Mbowe, kushindwa kusimamia katiba ya chama hicho katika kutatua migogoro, badala yake wakitumia na kuamini kuwa kufukuza wanachama tena kwa majungu ndio suluhisho la kukijenga na kukiimarisha chama.
Lakini pia walilalamikia chama hicho kujaa utashi wa nguvu ya umma na kulazimisha maandamano, migomo vitu ambavyo si vya lazima na kwamba kamwe hiyo si njia sahihi na malengo ya kweli ya kutafuta ukombozi.

Naye mmoja wa kada Chadema, Emanuel Mwangoka (Cash Money), ambaye inadaiwa kuwa ndiye alikuwa mfadhili Mkuu wa mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (Chadema), akikabidhiwa kadi ya chama kipya, alisema atatumia uwezo wake wote kama alivyofanya kwa sugu kuhakikisha NCCR-Mageuzi inaibuka na kung’ara mkoani hapa.
Kwa upande wake aliyewahi kuwa Katibu wa Chadema Mkoa wa Mbeya na kujiunga na NCCR-Mageuzi , Januari 20 mwaka huu Eddo Mwamalala, alisema wanachama hao waliomfuata ni mtaji mkubwa wa kuhakikisha inakimaliza chadema mkoani hapa.



Na Moses Ng’wat, Picha na Mbeya yetu

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake