Saturday, February 2, 2013

Samba Ataka Amani Kenya



Mwanamuziki anayekubalika sana Afrika Mashariki kwa kazi zake ambazo wakati wote zinakuwa zimebeba ujumbe mzito wa mafundisho, Samba Mapangala amerekodi wimbo maalum unaojulikana kama Chagua, kwa ajili ya kuwahamasisha wakenya kushiriki katika uchaguzi wao kwa amani pamoja na kuchagua viongozi makini.
Ujumbe wa msanii huyu ambao umepakiwa katika kibao kikali cha miondoko ya "Sokous" kwa mujibu wake mwenyewe, ni mchango wake katika kuhamasisha amani nchini Kenya, nchi ambayo ndipo mahali alipokulia.
Kazi hii imerekodiwa huko Arlington, Virginia pamoja na Paris, na tayari imeshaanza kusambazwa kwa njia ya mtandao, na ujumbe wake pia ni wa manufaa kwa nchi nyingine za Afrika ambazo mara nyingi hupitia hali zinazofanana hasa nyakati za uchaguzi mkuu.


No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake