Saturday, February 2, 2013

TANZANIA MISSION NEW YORK CITY WAMUAGA H.E BALOZI MWANAIDI MAAJAR

Mh. Balozi Tuvako Manongi wa Tanzania Mission New York City akiongea machache katika hafla fupi ya kumuaga Mheshimiwa balozi Mwanaidi Sinare Maajar anayemaliza muda wake. Hafla hiyo iliandaliwa na maofisa wa ubalozi wa New York City ilifanyika Ubalozini hapo, na kuhudhuliwa na viongozi wa NYTC.  
Mh. Balozi Mwanaidi Maajar akitoa shukrani zake katika hafla hiyo mbele ya wafanyakazi na maofisa wa Tanzania Mission New York. kushoto ni Balozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa New York,Mh. Balozi Tuvako Manongi kati ni Bwn. Shariff Maajar, Mume wa Mhe. Mwanaidi Maajar
Mh. Naibu balozi muwakilishi Ramadhani Muombwa Mwinyi akiongoe machache katika hafla hiyo
Wapili toka kulia ni Mgeni mualikwa H.E. Dr Elmi Ahmed Duale, Balozi wa Somalia upande wa United Nation New York katikati akiwa na mama mwenye nyumba wake.
Wageni waalikwa katika hafla hiyo wakipata vinywaji
Mhe. Balozi Mwanaidi Maajar katikati akiongea kwenye hafla hiyo ya kuagwa kwake, Kulia kwake ni Mhe. Balozi Manongi na kushoto kwake ni Mhe. Balozi Ramadhani Mwinyi.
Wafanyakazi wa Tanzania Mission pamoja na wageni waalikwa wakisikiliza hotuba fupi iliyokuwa inatolewa na Mh. Balozi Mwanaidi Maajar
Mwenyekiti wa Tawi la CCM New York Bwn. Masoud Maftah akiisalimia na waheshimiwa
Mkuu wa wilaya ya Springfield, Massachusetts (MA) Bwn. Isaack Kibodya alikuwepo na katika hafla hiyo hapa akijitambulisha na kusalimia kwa waheshimiwa.
Huyu ndiye alikuwa mshereheshaji wa hafla hiyo dada Tuly mfanyakazi wa Tanzania Mission New York City.
Mgeni mualikwa akisalimia waheshimiwa
Mhe.  Balozi Manongi akimkabidhi zawadi Mhe. Balozi Mwanaidi Maajar zawadi hiyo maalum kutoka kwa wafanyakazi wa Tanzania Mission New York.
Mhe. Naibu balozi akiifungua zawadi hiyo 
Mhe.  Balozi Manongi akishia zawadi hiyo baada ya kufunguliwa
Hajji Khamis mwenyekiti wa NYTC akiinua zawadi kabla ya kumkabizi Mhe.  Balozi Mwanaidi Maajar. Zawaidi hiyo imetolewa na Viongozi wa NYTC
Hajji Khamis akimkabizi zawadi Mhe.  Balozi Mwanaidi Maajar pamoja na bahasha yenye karatasi ya mashairi hayo yaliyotungwa na Hajji maalum kwa balozi
Hajji Khamis Mwenyekiti wa NYTC akisoma shairi hilo mbele wa Mhe.Balozi
Picha ya pamoja ya Viongozi wa NYTC na waheshimiwa
Mshereheshaji namba mbili katika hafra nae ni mfanyakazi wa Tanzania Mission New York.
Picha ya pamoja ya waheshimiwa, Mhe. Balozi Manongi mwanzo akifuatiwa na Mhe. Balozi Mwanaidi Maajar, Mhe. Balozi Elmi Daule na Mhe. Naibu Balozi Mwinyi.
Mhe. Balozi Tuvako Manongi, Mhe. Balozi Mwanaidi Maajar na Mhe. Naibu Balozi Ramadhani Mwinyi.

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake