FEBRUARY 14,2013
Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Nchini TPBC inewataka mabingwa wake wote wawe wametetea mikanda yao ya ubingwa ifikapo tarehe 30 Marchi kwaka huu ili kuepuka kunyanganywa.
Kwa kipindi kirefu mabingwa kadhaa wamekuwa wanakaa na mikanda bila kuitetea. Tunataka ieleweke kuwa muda wa kukaa na ubingwa wa TPBC ni miezi sita (6) tu na sio mwaka mmoja.
Bingwa wa kweli anatakiwa awe anafuata sheria, kanuni na taraibu za ubingwa alionao na sio kujiita bingwa wakati hufuati masharti yaliyowekwa.
Katika kipindi hiki cha mwaka 2013 tunawataka mabondia waheshimu sheria za mikataba wanayotiliana sahihi na mapromota. Tunataka ngumi ziboreshwe kakini pamoja na changamoto nyingi zilizoko, ikiwa ni pamoja na ukosefu wa wadhamini, mabondia wakiheshimu mikataba yao mchezo wa ngumi utakua na kuwavutia wadhamini.
Tunapenda pia kuwaomba wenye mapenzi mema na nchi hii wajitolekeze kwa wingi ili kushirikiana na sisi tuiweke Tanzania kwenye chati ya dunia kama zilivyo nchi nyingine.
Imetolewa na:
Onesmo A.M. Ngowi
Rais,
TPBC
Dar-Es-Salaam, Tanzania
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake