Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Charles Kenyela
Mtuhumiwa wa ujambazi, Omary Said (37), ameuawa kwa kipigo kutoka kwa wananchi wakati akiwa kwenye tukio la kijambazi na wengine 21 wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni, kwa tuhuma za ujambazi.Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Charles Kenyela, alisema marehemu, mkazi wa Tabata Aroma, aliuawa baada yeye na wenzake kumvamia, Abdulrahaman Mohamed, maeneo ya Mlimani City na kumpora fedha taslimu Sh. milioni 14 alizokuwa amezibeba kwenye mfujo wa rhambo.
Kamanda Kenyela watuhumiwa wengine kumi waliokamatwa kwa kutumia silaha katika maeneo ya Kawe, Kilima hewa, Boko Yombo Dovya, Tegeta, Mbezi Beach, Kunduki Mtongani na Ununio.
Aliwataja kuwa ni Alex Msale (27), Godfrey Msale (30), Harod Francis (26), Athuman Athuman (21), Isaya Songo (32), Magret John (30), Emanuel Thomas (28), Rukia Mohamed(26), Hamisa Mahamood (28) na Kelvin Mwehombe (24).
Walikamatwa wakiwa na bastola aina ya Browning yenye namba A 558656 iliyokuwa na risasi moja na Aina ya Astra yenye namba 1273826 iliyokuwa na risasi saba kwenye magazine.
CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment