Dar es salaam. Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zipo mbioni kuanzisha mchakato wa kuandaa mfumo wa pamoja wa Elimu na Mitalaa, itakayosaidia wananchi wa nchi hizo kupata nafasi za ajira katika nchi yeyote mwanachama.
Mbali na mchakato huo, tayari nchi hizo zimeshapitisha mfumo wa kisheria utakaowezesha nchi wanachama kuwa na mfumo wa pamoja wa utambuzi wa sifa za elimu na taaluma mbalimbali ndani ya jumuiya hiyo.
Akifungua Kongamano la Biashara la Wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Afrika Mashariki jijini Dar es Salaam jana, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Uledi Mussa alisema kuwa hatua hiyo itawapa uhuru wananchi wa nchi wanachama kufanya kazi na shughuli nyingine za kibiashara katika nchi yeyote Afrika Mashariki.
“Hatua hii itasaidia wananchi kutoka nchi wanachama kuvuka mipaka na kwenda kutafuta kazi na shughuli yeyote katika nchi wanachama bila kupewa visingizio vya kuwa elimu yake haiendani na mfumo wa elimu wa nchi anayoombea kazi” alibainisha Mussa.
Alisema licha ya kuwa hivi sasa kuna mifumo tofauti ya elimu na mitalaa katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, bado vijana wanatakiwa kupewa taaluma na ujuzi utakaowawezesha kupambana na changamoto za ukosefu wa ajira.
Alisema kuwa familia na jamii kwa jumla wanatakiwa kuwapa vijana mahitaji binafsi yaliyojengeka katika misingi ya kimaadili jambo litakalowasaidia kufa nya kazi na kuishi katika maisha mazuri.
Naye Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Nairobi cha nchini Kenya, Michael Megoh alisema kwamba mfumo wa elimu wa nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unawapa shida wanafunzi wengi pale wanapotaka kusoma katika baadhi ya vyuo katika nchi hizo.
Mshiriki wa kongamano hilo
rian Matara alisema mitalaa mingi ndani ya nchi za EAC haipitiwi mara kwa mara ili kwenda na wakati na kwamba kuna haja ya kuandaa mfumo wa elimu na mitalaa itakayoongeza ujuzi.
Mwananchi
No comments:
Post a Comment